In the News Room
The Web Kilimo web
Home | Budget Speeches | Publications | Agricultural Statistics | Legislations and Regulations | Web Links
 

TIZEBA : FANYENI KAZI KWA KUSHIRIKIANA

Waziri Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Dr. Charles John Tizeba amewataka wafanyakazi wa wizara yake kufanya kazi kwa ushirikiano ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Mhe. Dr. Tizeba alitoa wito huo wakati akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo wa wizara hiyo katika siku yake ya kwanza alipofika wizarani kuanza kazi rasmi.
“Kufanya kazi kwa pamoja tutaweza kufikia malengo yaliyokusudiwa , kitendo cha kutoshirikiana ndani ya wizara haitatufikisha po pote’’ alisitiza Mhe. Dr. Tizeba.
Mhe. Dr. Tizeba pia aliwataka watumishi wote ndani ya wizara kufanya kazi kwa kutoa ufumbuzi na majibu ya changamoto mbali mbali pasipo kumtegemea yeye kwa kuwa hana majibu kwani wao ndio watalaamu.
Aliwatahadharisha kutopeleka madokezo yenye kutafuta ufumbuzi kwake vinginevyo atachukua hatua kali.
‘’ Nawaomba mniandikie ushauri na si kuniandikia kutaka majibu toka kwangu, nyie ndo watalamu” aliongeza Mhe. Dr. Tizeba.
Tuwe watu wa kutoa majibu katika changamoto zetu na si kuningoja mimi nitoe majibu mie si mtalaamu.
Kitu kingine alichoongelea Dr. Tizeba ni kufanya kazi pasipokuwa na nidhamu ya uoga.
Aliongeza kuwa watu wenye nidhamu ya uoga huwa wanatoa ushauri ambao si sahihi kutokana na kuwa wamejaa hofu katika utendaji wao wa kazi.
‘’ Nisingependa kuwa na watu wenye tabia ya uoga tuwe huru na kupeana heshima inayostahili kuliko kuwa na nidhamu ya uoga’’ alifafanua Mhe. Dr. Tizeba.
Mwishoni mwa wiki Mhe. Rais Dr. John Pombe Magufuli alimteua Mhe. Dr. Charles John Tizeba, Mbunge wa Buchosa kuwa Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi kuchukua nafasi ya Mhe. Mwigulu Lameck Nchema aliyehamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani.

 

SIKU YA WAKULIMA WA MPUNGA MAKIFU YAFANA

Juhudi za Serikali kuzalisha mpunga kwa Wingi zimeanza kuonekana kwa wakulima wa kijiji cha Makifu, Wilaya ya Iringa, katika mkoa wa Iringa. Hali hiyo ilijidhihirisha katika maadhimisho ya siku ya wakulima iliyofanyika kijijini hapo katika skimu ya umwagiliaji ya Makifu. Katika siku hiyo Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bi. Wamoja Ayoub alikuwa mgeni rasimi.

 

Katibu Mkuu Kilimo DK. Florence Turuka, amezindua Mradi:


Katibu Mkuu Kilimo DK. Florence Turuka, amezindua Mradi wa kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga. Uzinduzi huo umefanyika kijiji cha kigugu wilaya ya Mvomero. Aidha, alitembelea shamba la mfano la mpunga la wakulima ambao walipatiwa mafunzo katika chuo cha Mkindo. Matumizi ya Teknolojia ya shadidi ni muhimu katika kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga.

 

MKUTANO WA WADAU WA MBOLEA:


Mkutano wa wadau wa mbolea uliitishwa kwa lengo la kupitia mapendekezo ya kurekebisha kanuni za mbolea. Mkutano huo ulifunguliwa na Katibu Mkuu Kilimo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Dk. Florence Turuka. Katika hotuba ya ufunguzi, alisisitiza umuhimu wa kuwashirikisha wadau katika kufikia muafaka wa kanuni zitakazosaidia kuboresha biashara ya mbolea hapa nchini.

 

MBEGU MPYA ZA MAZAO MBALIMBALI ZAIDHINISHWA


Kamati ya Taifa ya Mbegu (National Seed Committee) imeidhinisha matumizi ya aina 29 za mbegu mpya za mazao mbalimbali ya kilimo, mazao hayo ni mahindi,mpuga,alizeti karanga na chai.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Nchemba kwa vyombo vya habari, inasema kuidhinishwa kwa aina hizo za mbegu kunafuatiwa mapendekezo yaliyofanywa na kamati ya Taifa ya kupitisha aina mpya ya mbegu za mazao (The National variety Release Committee) katika kikao kilichofanyika kuanzia tarehe 16 – 17 Machi 2016, makao makuu ya Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Jijini Dar es salaam.
Aidha, aina hizo mpya za mbegu zimefanyiwa utafiti na kugundulika kuwa zinasifa mbalimbali ikiwemo kustahimili ukame,kutoa mavuno mengi,ukinzani dhidi ya magonjwa na wadudu,kukomaa mapema na kupendwa na wakulima.
Mhe. Nchemba aliongeza kuwa utafiti wa kina ulifanywa na vyuo vya utafiti vipatavyo12 na kuweza kuzalisha aina mpya za mbegu hivyo kupatikana aina 16 za mahindi,2 za mpunga, 4 za alizeti, 3 za karanga na 4 za chai.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa aina hizo za mbegu zitaanza kuzalishwa na makampuni mbalimbali ya uzalishaji mbegu pamoja na Wakala wa Taifa wa mbegu za kilimo (Agriculture Seeds Agency-ASA), kwa lengo la kuzifikisha aina hizo mpya za mbegu bora kwa wakulima kuanzia msimu ujao wa kilimo 2017/2018.
“ Hatua hiyo ya kamati inalenga kuongeza tija na kipato kwa mkulima”, iliongeza sehemu ya taarifa hiyo ya Mhe. Nchemba.

 

WAZIRI NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA IRELAND NCHINI


Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Chemba amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ireland nchini Tanzania Bi. Fionnuala Gilsenan ofisini kwake katika jitihada zake za kuinua sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.
Waziri Nchemba alimweleza Balozi huyo kuhusu hali ya sekta ya kilimo na mikakati ya serikali katika kukabiliana na changamoto zinazokikumba kilimo chetu hapa nchini ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa mbegu, ambapo vituo vya utafiti vya serikali na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) vimejikita katika kutafiti mbegu mbali mbali.
“Serikali imejipanga kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa mbegu bora kwa wakulima wetu” alieleza Mhe. Chemba.
Pia alisema kuwa uzalishaji wa mbegu bora na hasa za viazi utasukumwa kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji ili ziweza kupatikana kwa wakati kwa wakulima wetu.
Upatikanaji wa uhakika na kwa wakati wa mbolea kwa wakulima ni moja ya mikakati ya Serikali katika kuboresha na kuinua kilimo.
Mikakati mingine kwa mujibu wa Waziri Nchemba ni kwa upande sekta ya mifugo ambapo kuna changamoto ya kuwabadilisha wafugaji kutoka ufugaji wa kiasili na kuingia katika ufugaji wa kisasa.
Jitihada nyingine ni kuwaingiza vijana katika ufugaji wa kisasa wa samaki kwa kuwawezesha kupata zana bora za uvuvi, alibainisha Mhe Nchemba.
Balozi Bi. Gilsenan alimfahamisha Waziri Nchemba kuwa nchi yake imedhamiria kusaidia kuinua tija kwa kuboresha mnyororo wa thamani ya mazao.
Sehemu nyingine muhimu kwa mujibu wa Bi. Gilsenan ni pamoja na huduma za ugani, hifadhi na matumizi bora ya ardhi yanayolenga kupunguza migogoro, na kuchochea upatikanaji wa masoko kwa mazao yanayozalishwa.
Naye Mratibu wa Kitengo cha Mahusiano na Misaada ya Kimataifa kwa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Bi. Margareth Ndaba ameainisha maeneo ambayo Ireland inaweza kusaidia kuwa ni pamoja na lishe, Kilimo cha mboga mboga, zana za kilimo, utafiti na viwanda vya maziwa ili kusaidia kuondoa umaskini kwa Watanzania.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maabara ya Mifugo , Tanzania Dkt. Furaha Mramba alianisha changamoto ambazo Ireland inaweza kusaidia katika kuendeleza mifugo kuwa ni mabadiliko ya tabianchi ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa katika kuibua magonjwa mapya ya mifugo.
“Tunaomba Ireland kusaidia katika chanjo za mifugo ili kupambambana na magonjwa yanayoambatana na mabadiliko ya tabianchi” , alisisitiza Dkt Mramba.
Wakati huo huo Waziri Nchemba alikutana na wadau wa kilimo cha viazi kutoka Finland wakiongozwa na Naibu Balozi wa Finland nchini, Bwana Simo – Pekka Parviainen ambapo walimweleza nia ya kutaka kujikita katika kuboresha kilimo cha viazi mviringo.
Naye Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Peruna Mestant Bwana Aero Pisila alimfahamisha Waziri kuwa tayari wametembelea Mkoa wa Mbeya, Njombe na Arusha ili kuona fursa ya kuinua kilimo cha viazi mviringo na hasa kwa vijana wa Tanzania.
Aidha, Mratibu wa Mradi wa Kuendeleza kilimo cha Viazi Mviringo hapa nchini Bi. Matilda Byanda alifamweleza Waziri kuwa tayari wamefanya ziara za kujitambulisha katika Mikoa husika na kuonana na viongozi wa serikali na watalaam wa kilimo katika ngazi za halmashauri na kanda husika.
Waziri Nchemba aliwataka kubainisha maeneo ambayo serikali itachangia katika kutimiza lengo hilo la kuboresha kilimo cha viazi mviringo.

 

WIZARA YA KILIMO MIFUGO NA UVUVI

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUWATUMIA WAHITIMU WA VYUO VYA KILIMO WALIOSOMA KOZI MAALUM
Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi inautangazaia umma kuwa wahitimu mahiri 10,629 waliofuzu Vyuo vya Kilimo vya Inyala, Mtwara, Horti Tengeru, Igurusi, Katrin, Ukiriguru, Maruku, Uyole, KTC Moshi, Mlingano, Tumbi, Ilonga, NSI Kidatu na Mubondo, wanaweza wakatumiwa kwa lengo la kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo.
Jumla ya wahitimu 7,525 wamefaulu katika ngazi ya Astashaada kati ya hao, wanawake ni 2,557 na wanaume ni 4,968. Wahitimu 3,104 wameafaulu katika ngazi ya Stashahada (Diploma) ambapo wanawake ni 774 na wanaume 2,370.
Wahitimu hawa ni mahiri katika michepuo ya Stashahada ya fani ya kilimo cha mboga matunda na maua (Horticultural Crops), Zana za Kilimo, Uzalishaji wa Mazao, Umwagiliaji na Huduma za Kiufundi, Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi ya Kilimo na Chakula na Lishe.
Aidha, Wahitimu hao wanauwezo wa kiutendaji katika kuanzisha na kutunza bustani za mimea, mboga na matunda, kushauri wakulima kwa kutumia teknolojia mbalimbali ikiwemo TEHAMA, kusimamia kazi zote zinazohusu matumizi ya Zana za Kilimo na kuzifanyia matengenezo kila itapohitajika, kujenga miundombinu ya shamba ikiwemo maghala, vihenge na mabanda ya wanyama mbalimbali.
Pia wanauwezo wa kuzalisha mazao makuu ya chakula na biashara yanayolimwa nchini, kusaidia tafiti na kukusanya takwimu za utafiti wa mazao, kusimamia ujenzi wa miradi midogo ya umwagiliaji na kuandaa michoro ya miradi hiyo.
Wahitimu hao pia wanao uwezo wa kuandaa mazao baada ya kuvunwa, kuchakata na kufungasha, kufanya tathmini ya lishe na mahitaji ya chakula katika jamii, kuandaa mipango na kutoa ushauri kwa jamii kuhusu masuala ya lishe.
Serikali inawafahamisha Wadau wa maendeleo ya kilimo na mifugo, Wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi na yeyote mwenye mahitaji yanayoweza kutekelezwa na wataalam hawa kuwa wanayo fursa ya kuwaajiri, wahitimu hao ili kupata ufanisi katika shughuli zao za kilimo.

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA KILIMO MIFUGO NA UVUVI
18/01/2016

 

Waziri Nchemba atoa wito kwa wakulima wa mihogo kuchangamkia fursa ya kuzalisha zao hilo kwani soko lipo ndani na je ya nchi


Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na Balozi wa Ubelgiji nchini Bwana Paul Cartier
na kulia kwa Balozi ni Afisa kutoka Ubalozi huo Bibi. Isabelle Wittoek


Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba alitoa wito huo kwa Wakulima waktia wa mazungumzo ya kikazi na Balozi wa Ubeligiji nchini Mheshimiwa Paul Cartier wakati alipomtembelea ili kujitambulisha na kumpongeza.
Waziri Nchemba alisema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na mkazo umewekwa kuongeza uzalishaji na uongezaji wa thamani mazao ya kilimo.
Waziri Nchemba alimwambia Balozi Cartier kuwa Serikali imedhamiria kubadilisha hali ya uchumi ya Watanzania wa kipato cha chini na cha kati na kwa maana hiyo mkazo ni kuongeza uzalishaji ambao kwa kipindi kirefu umekuwa ndiyo tatizo.
Waziri Nchemba amesema kwenye suala la ubora kwa zao hilo si tatizo kwani Serikali kupitia Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi imejenga mahabara ya kisasa kwa ajili ya kuzalisha vipando bora na kwamba watafiti katika Kanda ambazo mihogo imekuwa ikizalishwa, wamekuwa wakizalisha vipando bora na vya kutosha kwa ajili ya kutosheleza wakulima wengi.
Waziri Nchema alimuakikishia Balozi huyo kuwa Mikoa ya Pwani, Kanda ya Ziwa na Ukanda wa Ziwa Tanganyika uzalishaji utaongezeka mara dufu kwamba ni nafasi ya Wakulima kuchangamkia fursa ya kulima zao hilo kwa wingi kwani soko lipo na uhakika.
Awali Bibi Margareth Ndaba Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Kimataifa, Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi alimueleza Waziri Nchemba kuwa Tanzania imepokea maombi ya kuuza mihogo yake nchini China na kuongeza kuwa ni fursa kwa Wakulima wa Tanzania kuichanghamkia fursa hiyo kwani kiwango kinachotakiwa ni kikubwa ukilinganisha na uzalishaji

 

“TAFUTENI MAJAWABU YA KERO ZA WANANCHI”
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Awaagiza Watumishi!
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Mwigulu Lameck Nchemba amewataka wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, kutumia muda wao kuhangaikia kutafuta majawabu ya matatizo ya wananchi.  Aliyasema hayo wakati anaongea na Wakuu wa Idara za kilimo, mifugo na Uvuvi mara baada ya kuwasili Wizarani hapo kufuatia alipoteuliwa kuiongoza Wizara hiyo.

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Mwigulu Lameck Nchemba (Kushoto) wakati anawasili Wizarani. Katikati ni Katibu Mkuu, Bibi Sophia Kaduma, na Kulia ni Katibu Mkuu Dk. Yohana Budeba

Katika hotuba yake aliyoitoa baada ya kukabiribishwa na Wafanyakazi wa Wizara hiyo, Mheshimiwa Waziri alionya kuwa hizi siyo zama za kufanya kazi kwa mazoea ambapo kila mtumishi anatakiwa kusugua kichwa kutafuta majawabu ya kero za wakulima, wafugaji na wavuvi ambao ni zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania.
Alisema, ipo dhana iliyojengeka miongoni mwa watumishi wa Serikali kuwa muda mwingi wanahangaika kutafuta “majibu” badala ya “majawabu” ya matatizo yanayo wakabili wananchi. Akitoa mfano wa maelezo yake alisema, pembejeo za kilimo zinapochelewa kufika kwa wakulima jibu linaweza kutolewa kuwa makampuni na wakala wa pembejeo hawakupeleka mbolea kwa wakati. Hilo linaweza kuwa ni jibu lakini siyo jawabu au suluhisho la tatizo kwa wakulima ambao wameshindwa kutumia mbolea kuendena na msimu wa kilimo.
Katika hotuba yake, aliwataka watumishi katika kila eneo kupitia kero zinazowakabili wananchi na kuweka mikakati ya kuzishughulikia kero hizo katika muda mfupi.
“Nataka katika kipindi cha siku saba muainishe kero na mikakati yake ya kuzitatua ili tupate matokeo kwa haraka” alisema Mheshimiwa Nchemba.

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Mwigulu Lameck Nchemba (katikati), akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wakuu wa Idara za Kilimo, Mifugo na Uvuvi (hawapo pichani)

Katika moja ya mambo yanayotakiwa kushughulikiwa kwa haraka ni pamoja na kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo inazidi kukua kila siku kwa kuzingatia kuwa ardhi haiongezeki, hali ya hewa inabadilika, wakati watu na mifugo inaongezeka.  Hivyo, lazima hili tatizo lipatiwe suluhisho kwa haraka na kama kuna kitu  kinakwamisha lazima kielezwe ili kiondolewe,  alisema Mheshimiwa Nchemba.  
Mheshimiwa Nchemba alihitimisha, kwa kuwataka watumishi kujituma na kufanyakazi kwa ushirikiano wa hali ya juu ili kupata mafanikio yanayohitajika.
Naye, Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Olenasha alisema, falsafa ya utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano, ni kufanya jambo kwa haraka, kwa wakati na kupata matokeo sahihi na tija kwa kuzingatia maslahi mapana kwa umma.
Alisema, mathalani unapolima shamba, kazi inakuwa imefanyika, lakini kinachotegemewa ni kupata mavuno ambayo mwisho wa siku yatatumika kuwapatia chakula Watanzania.  Aliwataka wafanyakazi wa Wizara hiyo kuzingatia falsafa hiyo wanapotekeleza majukumu yao ili mwisho wa siku wananchi waone mabadiliko katika maisha yao.
Mara baada ya kuwasili Wizarani hapo, Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri walipokea maelezo ya shughuli za kilimo yaliyotolewa na Katibu Mkuu Bibi Sophia Kaduma, ambapo maelezo ya shughuli za Mifugo na Uvuvi yalitolewa na Katibu Mkuu Dk. Yohana Budeba. 

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Mwigulu Lameck Nchemba (wa tisa kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi

Waziri na  Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi

     
Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb)                            Mhe. William Tate Ole Nasha (Mb).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza Baraza jipya la Mawaziri ambalo lina jumla ya Mawaziri 19 na Naibu Waziri 15.

Katika Baraza hilo, iliyokuwa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika imeunganishwa na iliyokuwa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na kuwa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi.

Katika Baraza hilo jipya la Serikali ya Awamu ya Tano lililotangazwa, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekuwa Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, wakati Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, ni Mhe. William Tate Ole Nasha (Mb).

Watumishi wa Wizara wamepongeza na kuwakaribisha sana Viongozi hao Wakuu.

Wakiongea kwa nyakati tofauti, Bwana Rashid Likiligo wa Kitengo cha Mifumo ya Kopyuta, amesema, “Uteuzi aliofanya Mhe. Rais Magufuli ni mzuri na umelenga kuleta ufanisi katika Wizara hasa kwa kuzingatia uchapakazi wa viongozi hao”.

Naye Caltas Kabyemela wa Idara ya Utafiti na Maendeleo alisema, “Nimependa uteuzi huo, hao wote waliochaguliwa ni wachapakazi na naamini Wizara yetu mpya itafanikiwa na kuwa na maendeleo yatakayoonekana kwa wananchi ambao ni zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania”.

 

IMPORTANT NOTICE

Dear valued customer,
This website is undergoing reorganization following changes in the Government Ministries announced recently by the President of the Fifth Phase Government of the United Republic of Tanzania, Honourable Dr. John Pombe Joseph Magufuli.  The changes will include the amalgamation of the former two Ministries of Agriculture Food Security and Cooperative; and Livestock and Fisheries Development which has now become the Ministry of Agriculture Livestock and Fisheries.
In the changes, the current Minister for Agriculture Livestock and Fisheries is Honourable Mr. Mwigulu Lameck Nchemba, (MP), whereas the Deputy Minister is Honourable Mr. William Tate Ole Nasha, (MP).
In the meantime, and for the public interest, the websites under the former ministries will continue as they are until harmonization into one website is completed. Thank you for your understanding.

 

 

Serikali Yaongeza Idadi ya Maafisa Ugani

Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo, Wizara Kilimo Chakula na Ushirika Bibi Anne Assenga amesema katika msimu wa kilimo wa 2014/2015 Serikali imefanikiwa kuongeza idadi ya Maafisa Ugani na kufikia 11,073 walioajiriwa ikilinganishwa na lengo la kufikia Maafisa Ugani 15,082 ifikapo mwaka 2020.

Bibi Assenga alibainisha hayo wakati akiongea na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, ofisini kwake hivi karibuni na kuongeza kuwa lengo la Serikali ni kuwa na Maafisa Ugani katika kila kata na Kijiji.

Bibi Assenga aliongeza kuwa, Serikali imekuwa ikiongeza idadi ya wanafunzi katika Vyuo vya Kilimo na kwa sababu hiyo Maafisa Ugani wamekuwa wakiongezeka kila mwaka. Hali hiyo imewezesha kila Kata hapa nchini kuwa na Afisa Ugani ukiacha Kata mpya zilizotokana na Serikali kutangaza Mikoa na Wilaya mpya mapema mwaka jana.

Aidha, Bibi Assenga aliongeza kuwa kuongezeka kwa idadi hiyo ya Maafisa Ugani imetokana na Serikali kuweka mkazo wa kusomesha vijana wengi katika Vyuo vya Kilimo sambamba na Vyuo binafsi  kudahiri wanafunzi wengi katika fani ya kilimo.

Bibi Assenga alivitaja Vyuo hivyo binafsi vinavyotoa mafunzo ya fani ya kilimo katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kuwa ATI Kilacha (Moshi), St. Maria Gorette College of Agriculture (Iringa), ATI Igabilo (Kagera), College of Agriculture and Natural Resources, CANRE (Dar es Salaam), Mount Sinai Teachers College (Dar es Salaam), Kaole College of Agriculture (Pwani), MAMRE Agriculture and Livestock College (Njombe), Dr. Clement Fumbuka Memorial College (Mwanza) Dabaga Institute of Agriculture (Iringa).

Vyuo vingine ni TRACDI (Dodoma), Mbalizi Polytechnic College (Mbeya) Katavi Polytechnic College (Katavi) na Mbeya Polytechnic College (Mbeya).

Bibi Assenga aliongeza kuwa Wizara inashirikiana na Vyuo binafsi kutoa mafunzo ya kilimo katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa kutumia mtaala wa pamoja kwa lengo la kuwa na uelewa wa pamoja na kukidhi viwango vinavyokubalika Kitaifa na Kimataifa.

Aidha, Mkurugenzi huyo wa Idara ya Mafunzo alisema katika muhula mpya wa masomo ulioanza Mwezi Septemba, 2015 katika Vyuo vya Serikali jumla ya wanafunzi 2,596 walidahiriwa ambapo katika idadi hiyo wanaume ni 1,603 na wasichana ni 993.

Katika mwaka wa masomo uliopita jumla ya wanafunzi 453 walidahiriwa, ambapo wanaume walikuwa 291 na wanawake walikuwa 162.  Bibi Assenga alihitimisha kwa kutoa wito kwa vijana wote wanaopenda kujiunga na Vyuo vya Kilimo kujiandaa na muhula mpya ambao maombi yataanza kupokelewa kuanzia Mwezi Mei, 2016.

 

Makampuni ya Pembejeo Fikisheni Pembejeo Haraka kwa Wakulima - Katibu Mkuu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Bibi Sophia  Kaduma  ameyahimiza Makampuni yanazoshiriki  kusambaza pembejeo kwa wakulima kwa kutumia  mfumo wa vocha katika msimu wa kilimo wa 2015/2016, kupeleka haraka pembejeo kwa wakulima hususan mbegu bora na mbolea,  kwa haraka kwa kuwa msimu wa kilimo umeanza katika maeneo mengi hapa nchini na kuongeza kuwa wanapaswa kufikisha pembejeo hizo hata katika maeneo ambayo msimu wa kilimo haujaanza.
Bibi Kaduma alisema hayo hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Kilimo 1 alipokutana na Wawakilishi wa Makampuni yanazosambaza pembejeo kwa kutumia mfumo wa vocha katika msimu wa kilimo wa 2015/2016.
Aidha Bibi Kaduma alisema, kwa kuzingatia mwongozo uliosambazwa kwa Makampuni hayo na Halmashauri za Wilaya, ya kuwa kila Kampuni, inapaswa kuwasilisha kwenye Halmashauri za Wilaya, orodha ya Mawakala iliyowateua na maeneo, watakayoyafanyia kazi, na  nakala yake iwasilishwe Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika. 
Bibi Kaduma pia, ameyatahadharisha Makampuni hayo kuteua Mawakala waaminifu, na si watakaowahadaa wakulima kwa kuwalipa fedha kidogo ili wasaini vocha bila  kupewa aina yoyote ya pembejeo.
"Mawakala watende haki kwa wakulima, na Kampuni itakayofanya udanganyifu, itawajibika kwa jambo litakalohusiana na usambazaji wa mbegu feki , na mbolea zitakazokuwa chini ya kiwango”. Alisisitiza, Bibi Kaduma.
Bibi Kaduma alihitimisha kwa kuwahakikishia Wawakilishi wa Kampuni za pembejeo kuwa, Serikali itashirikiana nayo katika kufanikisha zoezi zima la usambazaji wa pembejeo kwa kutumia mfumo wa vocha katika msimu wa kilimo wa 2015/2016.

Katibu Mkuu aipongeza Benki ya Dunia kwa Kusaidia Mradi wa EAAPP

 

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Bibi Sophia Kaduma hivi karibuni aliwashukuru Wajumbe kutoka Benki ya Dunia kwa namna ambavyo Taasisi hiyo kubwa ya fedha Duniani, ilivyofadhiri na kufanikisha mradi wa EAAPP ambao, awamu ya kwanza itakamilika, 31 Desemba, 2015.
Bibi Kaduma alisema mafanikio, yaliyopatikana baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ya mradi huo, yamepokelewa na wakulima na wadau wa Sekta ya kilimo kwa mikono miwili na kusisitiza kuwa Tanzania inaunga mkono utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi huo kama fursa hiyo, itapatikana.
Bibi Kaduma alitoa pongezi hizo katika mkutano maalum mbele ya Wajumbe kutoka Benki ya Dunia na Wasimamizi wa mradi huo kutoka Tanzania ambao ni Idara ya Utafiti na Maendeleo, kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika  na Idara ya Mifugo,  kutoka Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi.
Mwakilishi wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bwana Abel Lufafa alimuhakikishia Katibu Mkuu kuwa Benki ya Dunia haitasita kuendelea kufadhiri awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi huo na kwamba ameomba wadau wa kilimo kusubiri kikao cha kupitisha maamuzi ya kuendelea na ufadhiri huo.
Bwana Lufafa alisema siku zote Benki ya Dunia ipo tayari kusaidia miradi yote yenye lengo la kuwasaidia wakulima, na hasa yenye kuleta tija na uzalishaji katika mazao ya kilimo na mifugo kwa kuwa suala ya kupambana na njaa ni kipaumbele cha kwanza.
Bibi Kaduma aliongeza kuwa moja kati ya mafaniko ya utekelezaji wa mradi wa EAAPP ni  kuongezeka kwa uzalishaji wa mbegu bora za mazao ya kilimo na kusisitiza kuwa Serikali itajitahidi kuwawezesha wakulima wanaozalisha mbegu bora kufanya biashara hiyo kwa uhakika,  wakiwemo wa ndani na nje ya nchi kwa kuwa Tanzania imeshakuwa mwanachama wa Shirika la Kimataifa la Hakimiliki za Wagunduzi wa Mbegu za Kilimo na Mimea mingine Duniani, (UPOV - International Union for the Protection of New Varieties of Plants).
Naye Mjumbe mwengine wa Benki ya Dunia, Dkt. Joseph Oryokot kutoka nchini Uganda alisema tayari nchi za Tanzania na Uganda zimeshawasilisha maombi ya kuiomba Benki hiyo kufadhiri mradi huo kwa awamu ya pili na kuongeza kuwa  suala la kilimo na uhakika wa chakula ni agenda ya muhimu kwao na kwamba bila shaka Taasisi yao italifanyia kazi ombi hilo.
Dkt. Oryokot alipongeza hatua ya Serikali ya Tanzania kuahidi kuwasaidia wakulima wake ili wauze mbegu zao nje ya mipaka na kusisitiza ni vyema nchi wanachama wakawa na sauti ya pamoja ya kuwasaidia wakulima kutengeneza mitandao ya masoko katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kwamba bila ya kufanya hivyo, wakulima wengi, wataendelea kukandamizwa na walanguzi ambao wapo kila mahali.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTATUZI WA MGOGORO WA WAKULIMA WA MIWA KILOMBERO


Bodi ya Sukari Tanzania imefuatilia na kubaini chanzo cha malalamiko ya wakulima wa miwa wanaozunguka Kiwanda cha Sukari cha Kilombelo (ILOVO).
Akizungumza katika taarifa yake, Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Sukari Tanzania Bwana Henry Semwanza alisema kuwa, chanzo cha malalamiko yanatokana na kiwanda kuharibika bila kutarajia na kusimamisha uzalishaji kuanzia tarehe 14 hadi 18 Novemba 2015.
Hali hiyo ilisababisha miwa ya wakulima ambayo ilikuwa imekatwa kuharibika na hivyo kukosa sifa ya kuchukuliwa na kiwanda kwa ajili ya usindikaji.
Bwana Semwanza aliongeza kuwa hali hiyo ilisababisha tani 250 za miwa kutoruhusiwa kuingia kiwandani kwa vile zilishapita zaidi ya siku tano tangu miwa ilipochomwa.
“Miwa hiyo ilichomwa tangu tarehe 14 Novemba 2015 siku ambayo kiwanda kiliharibika, na kilipotengamaa zilikuwa zimeshapita siku tisa, hivyo miwa hiyo kukosa sifa na ubora unaokubalika, na hivyo ikazuiliwa kuingia kiwandani”
Akizungumzia utekelezaji wa mkataba wa ugavi wa miwa baina ya Kampuni na Vyama vya Wakulima, Bwana Semwanza alibainisha kuwa Kifungu cha 5.2.3.3 cha mkataba huo kinasisitiza kutokuikubali miwa ambayo kiwango cha ubora wake uko chini ya asilimia 80 au miwa iliyopitisha siku tano tangu ilipochomwa kwa mujibu wa kifungu cha 5.2.3.4.
Ili kupunguza hasara inayoweza kutokea kwa wakulima, Bwana Semwanza aliwakumbusha wakulima na wamiliki wa kiwanda kuzingatia taratibu za uvunaji wa miwa.
“ninatoa wito kwa wakulima kupitia vyama vyao kuzingatia taratibu za uvunaji kwakuwa imedhihirika pasipo shaka kuwa baadhi wamekuwa wanavuna miwa mingi zaidi ya mgao wao wa siku, mambo haya yasipozingatiwa yanaweza kuibua migogoro isiyo ya lazima ” Bwana Semwanza alibainisha katika taarifa yake.
Aidha, alisisitiza kuwa kamati iliyoundwa chini ya mkataba wa ugavi wa miwa inayojumuisha wakulima na uongozi wa Kiwanda na ambayo hukutana kila siku iendelee kuwa msingi wa kuamua kiasi cha miwa inayotakiwa kuvunwa na kupelekwa kiwandani katika siku inayofuata.
Semwanza aliongeza kuwa Bodi yake inaendelea kufuatilia utekelezaji wa makubaliano kati ya kiwanda na wakulima, na haitasita kuchukua hatua sitahiki kwa upande utakao kiuka ili kutatua migogoro inayoweza kuzuilika kwa haraka.
Semwanza alisisitza kuwa kwa sasa hali ni shwali ambapo uvunaji na upokeaji wa miwa kiwandani unaendelea kama kawaida na wakulima wameongezewa mgawo wa miwa inayotakiwa kuingizwa kiwandani kila siku.
“hali ya uvunaji inaendelea kama kawaida na mgao wa wakulima kuingiza miwa yao kiwandani umeongezwa kwa zaidi ya asilimia 50; ili kuhakikisha miwa yote ya wakulima wanaozunguka kiwanda cha Kilombero inavuwa”
Bodi ya Sukari Tanzania inashirikiana kwa karibu na uongozi wa mkoa na Wilaya ili kushughulikia migogoro isiyo ya lazima. Alihitimisha Bwana Semwanza.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika
Kilimo Complex,
1 Mtaa wa Kilimo 15471
DAR ES SALAAM

 

Naibu Katibu Mkuu Afungua Mkutano wa Kanda wa Mradi wa EAAPP EAAPP


Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Eng. Raphael Daluti hivi karibuni alifungua mkutano wa 10 wa Mashariki mwa Afrika wa kuhitimisha awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa EAAPP.
Katika hotuba yake, Eng. Daluti alisema, kuna mambo mengi ya kujivunia kutokana na matokeo ya utekelezaji wa mradi katika kipindi cha miaka mitano huku akitaja maeneo ambayo yamekuwa na ongezeko la uzalishaji wa maziwa, mazao ya mpunga,  mihogo na ngano.
Eng. Daluti aliongeza kuwa eneo lililoonyesha mafanikio wakati wa utekelezaji wa mradi huo, ni ongezeko la wataalam katika eneo la utafiti. Mradi umefanikisha ufadhiri katika tafiti kadhaa na kuongeza kuwa zaidi ya Watafiti 110 kwenye ngazi mbalimbali walishiriki huku zaidi ya Watafiti 6 kwenya ngazi ya shahada ya uzamivu (PhD) na Watafiti 16 kwenye shahada ya Uzamili (Masters Degree) walifadhiriwa na kusoma kwenye vyuo mbalimbali.
Mafanikio mengine ni pamoja na kuongezeka kwa mshikamano wa Kikanda katika maendeleo ya sekta ya kilimo kwani kumekuwa na juhudi za pamoja za kukabiliana na changamoto zinazomkabili mkulima wa Afrika. Alipongeza juhudi hizi kuwa ni namna nzuri ya kujiandaa kukabiliana na ongezeko la idadi ya watu, ambapo, inafikiriwa kuwa ifikapo mwaka 2050 dunia itakuwa na watu zaidi ya bilioni 9.1 ambao watahitaji chakula ambacho kwa sehemu kubwa, kinazalishwa Afrika.
“Wote, tunafahamu namna ambavyo malengo ya mradi wa EAAPP yalivyotekelezwa kwa vitendo na matokeo, yameonekana kwenye, kuongeza tija na uzalishaji lakini pia kuongezeka kwa ushirikiano katika kuboresha teknolojia na mafunzo ya wataalam. Hayo yamechangiwa na jinsi ambavyo nchi zetu, zilivyoshirikiana katika upeanaji wa taarifa za kimkakati katika mazao manne ya kipaumbele ambayo, ni mpunga, ngano, mihongo na uzalishaji wa maziwa.” Alisema Eng. Daluti.
Mradi wa EAAPP ulikuwa ukitekelezwa na taasisi za kilimo na mifugo katika nchi nne ambazo ni Ethiopia, Kenya, Tanzania na Uganda kwa mazao ya ngano, maziwa, mpunga na muhogo.
Mradi huo ulikuwa na malengo ya kuzalisha teknolojia kupitia utafiti wa mazao ambayo ni ngano, mpunga, muhogo na maziwa, pia kuzisambaza kwa walengwa ambao ni wakulima na wafugaji.
Tangu mradi wa EAAPP ulipoanzishwa miaka minne iliyopita zaidi ya teknolojia 400 zimepatikana na kusambazwa kwa wakulima na wafugaji.
Akizungumza katika mkutano huo, mtalaam kutoka Kenya Dkt. David Wekesa Nyongesa alisema mradi huo umewawezesha kuzalisha mbegu za mifugo ambazo zimeanza kuwa na mahitaji makubwa ndani na nje ya Kenya.
Mradi wa EAAPP ulianza kutekelezwa mwaka 2010 na utafikia tamati ya awamu ya kwanza, tarehe 31, Desemba, mwaka huu.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UGONJWA WA MNYAUKO FUSARI WA PAMBA NA MBEGU ZISIZOOTA

 

Serikali imewataka wachambuaji na wasambazaji wa mbegu za pamba kuacha kuwasambazia wakulima mbegu zilizozalishwa katika maeneo yaliyobainika kuwa na ugonjwa wa mnyauko fusari (Fusarium Wilt Disease). Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Usimamizi, Bodi ya Pamba Tanzania, Bwana James Shimbe.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Bwana Shimbe amesema, ugonjwa wa mnyauko fusari unaweza kudhibitiwa ikiwa wakulima wa pamba watatumia mbegu bora kutoka kwa wasambazaji wanaotambulika na Bodi ya Pamba Tanzania.

Akizungumzia tatizo la kuenea kwa ugonjwa huo Bwana Shimbe amesema kwa kiasi fulani limetokana na baadhi ya wachambuaji wasio waaminifu kuendelea kusambaza mbegu za pamba za kupanda ambazo zinaweza kuwa zimetoka katika maeneo yaliyobainika kuwa na ugonjwa wa mnyauko fusari.

“Tulishatoa maelekezo kwa kuwataka wasambazaji wa mbegu za pamba za kupanda kutosambaza mbegu zilizozalishwa katika maeneo yenye ugonjwa.”

Hivyo tunaendelea kusisitiza kuwa wakulima wawe makini wanapo nunua mbegu kutoka kwa wasambazaji wasiotambulika na watoe taarifa haraka kwa Bodi wanapoona mbegu hizo hazioti ili hatua za haraka zichukuliwe za kupeleka mbegu zingine mbadala ili kuendana na msimu wa kilimo.

Aidha, Bwana Shimbe amewataka wachambuaji wa pamba ambao ndio wasambazaji wa mbegu kuacha mara moja kuwasambazia wakulima mbegu ambazo zimetoka kwenye maeneo yaliyobainika kuwa na ugonjwa na badala yake mbegu za pamba hizo zisindikwe kuzalisha mafuta ya kula kama walivyokuwa wameelekezwa na Bodi hapo awali.

“ Bodi ilishatoa maelekezo kwa wachambuaji wote wa pamba kote nchini, kutenga mbegu za pamba za kupanda msimu huu wa kilimo kutoka maeneo yaliyo salama kwa kuziwekea lebo ili kuzitofautisha na zile zinazotoka kwenye maeneo yaliyobainika kuwa na ugonjwa, ambapo zile zinazotoka katika maeneo yenye ugonjwa zisitumike kama mbegu za kupanda, bali zisindikwe kupata mafuta ya kula kama sehemu ya kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa, na zile mbegu ambazo zimetoka kwenye maeneo yasiyo na ugonjwa zisambazwe kwa wakulima kwa ajili ya kupanda kwenye mashamba yao baada ya kufanyiwa majaribio ya uotaji (seed germination test) na taasisi inayohusika na udhibiti wa ubora wa mbegu (TOSCI)”

Aidha, mbegu zinazofaa kutumika kwa sasa ni UKM08 iliyofanyiwa utafiti na Kituo chetu cha Utafiti cha Ukiriguru, ambayo ubora wake umethibitishwa na Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu (TOSCI) na inauwezo wa kuhimili magonjwa pamoja na uzalishaji wenye tija zaidi. Mbegu hiyo itakuwa inaiondoa kwenye uzalishaji ile ya zamani ya UK 91 ambayo imepungua ubora wake. Katika msimu huu wa kilimo wa 2015/16 Mbegu ya UKM08 itaendelea kuzalishwa kwa wingi (seed multiplication) katika maeneo salama yasiyo na ugojwa wa mnyauko fusari katika mkoa wote wa Singida na wilaya ya Nzega na Igunga, mkoa wa Tabora.

Bwana Shimbe ametoa wito kwa wakulima na wadau wote wa pamba nchini kufuata kanuni za kilimo bora cha pamba ikiwa ni pamoja na kutumia mbegu bora za pamba. Aidha, baadhi ya mawakala wa ununuzi wa pamba mbegu na wakulima wenye tabia ya kuchanganya pamba mbegu na maji, mchanga, chumvi na kemikali zingine kama vile “mafuta ya kenge” kwa madai ya kuongeza uzito kwenye pamba yao waachane na tabia hiyo potofu, kwani kwa kufanya hivyo kunachangia kuoza kwa kiini cha mbegu na kuharibu ubora wake na hivyo kusababisha mbegu kutokuota.

Imetolewa:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika
Kilimo Complex
1 Mtaa wa Kilimo 15471
DAR ES SALAAM

 

Uzalishaji wa zao la korosho waongezeka

Katibu Mkuu  Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bibi Sophia Kaduma amesema kuwa Tanzania imeweka rekodi mpya kwa kuzalisha karibu tani  200,000 za korosho katika msimu wa 2014/2015 ukilinganisha na tani 158,000 zilizozalishwa mwaka 2011.

“Kiwango hiki cha uzalishaji ni mafanikio chanya si tu kwa Wanasayansi na  Watafiti lakini pia katika mnyororo mzima wa thamani wa zao la korosho wakiwemo Maafisa Ugani, Wataalamu wa soko, wasambazaji wa pembejeo na wakulima” alifahamisha Bibi. Kaduma.

Pia Bibi. Kaduma alibainisha kuwa Tanzania ni nchi pekee Barani Afrika ambayo imefanya ugunduzi wa  aina mpya ya mbegu na mbegu chotara za korosho kwa kufuata viwango vya Kimataifa ambapo hadi sasa aina 16 zimeruhusiwa kutumiwa na wakulima na aina 22 zipo katika hatua za mwisho za utafiti. Aina hizo 16 za mbegu za korosho zinatoa mavuno mengi na zina kiwango bora cha punje na  tayari zinalindwa kisheria.

Aidha, Bi.Kaduma aliongeza kuwa Tanzania ni nchi pekee duniani inayouza korosho kwa kutumia mfumo wa Stakabadhi Ghalani ambao umechangia kupandisha bei kwa mkulima na kuongeza ubora wa korosho ghafi zinazozalishwa nchini.

 “Tanzania ni miongoni mwa nchi chache zilizoweka mfumo wa kuwawezesha Wadau kuchangia maendeleo ya Sekta ya korosho, moja ya mfumo huo ni kuanzishwa kwa Mfuko wa Wakfu wa  Kuendeleza zao la Korosho ambao ni kiungo muhimu katika mnyororo wa thamani wa zao la korosho,  kwani unachangia katika shughuli za utafiti,  kusambaza pembejeo kwa wakulima, usindikaji, soko na ubora” alifahamisha Bibi Kaduma katika hotuba yake.

Mfuko wa Wakfu wa Kuendeleza Zao la Korosho umepiga hatua kubwa kwa kuwawezesha wadau mbalimbali kwenye mnyororo wa thamani wa korosho kuwapatia mikopo na pembejeo.
Nchi zilizoshiriki katika mkutano huo ni pamoja na Kenya, Uganda, Nigeria, Ivory Coast, India, Burkina Faso na China.

Nchi nyingine ni Australia, Algeria, Pakistan, Zimbabwe, Sri Lanka, Cape Verde,  Marshall Island,  Malawi na mwenyeji wa mkutano huo Tanzania.
Mazingira.

Mkutano huo uliofanyika Jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Serena na uliandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele kwa kushirikiana na Bodi ya Korosho na Mfuko wa Wakfu wa Kuendeleza zao la Korosho (CIDTF)  na ulibeba  Kaulimbiu  isemayo Korosho kwa Afya, Utajiri na Mazingira.

 

Upatikanaji wa Vibali vya Kusafirisha Mazao Nje ya Nchi

 

Serikali leo imetoa ufafanuzi kuhusu upatikanaji wa vibali vya kusafirisha mazao kwenda nje ya nchi ambapo imesisitiza kuwa vibali hivyo vinapatikana bila gharama  na hakuna urasimu wowote.
Akitoa ufafanuzi huo, Mwanasheria wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bwana George Mandepo alisema kuwa vibali vya kusafirisha mazao ya kilimo nje ya nchi, hutolewa bila gharama na kuongeza kuwa biashara hiyo inaweza kufanywa na mtu yeyote, kinachotakiwa ni mhusika kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.
Bwana Mandepo aliongeza kuwa, uuzaji wa mazao nje ya nchi, unasimamiwa na Sheria ya Usalama wa Chakula iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009, inayojulikana kama Sheria ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (Serial and Other Produce Act, 2009) inayompa mamlaka Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika kutoa kibali cha kuuza mazao nje ya nchi kwa mtu mwenye vigezo.
Sheria hiyo pia, inampa mamlaka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, kukasimu madaraka ya kutoa vibali kwa Makatibu Tawala wa Mikoa wakati wa dharura kama ilivyokuwa katika msimu wa kilimo wa 2013/2014 ambapo Taifa lilikuwa na ziada ya kutosha.
Bwana Mandepo aliongeza kuwa, katika Sheria hiyo inamtaka mfanyabiashara kuainisha aina ya mazao na  kiwango ambacho anataka kusafirisha, lengo ni kuhakikisha kuwa, Serikali inakuwa na takwimu kamili za mazao yanayosafirishwa nje ya nchi.
Baadhi ya masharti nafuu ambayo mfanyabiashara anatakiwa, kuyafuata ni pamoja na kuwasilisha taarifa zake binafsi kama Jina lake kamili au Jina la Kampuni, anuani ya makazi, au eneo analotoka na uthibitisho wa mazao anayotaka kusafirisha nje ya nchi.
Aidha, Bwana Mandepo aliongeza kuwa Mfanyabiashara wa mazao kwenda nje ya nchi atapaswa kuwa na Cheti cha ubora wa mazao husika anayosafirisha, kinachojulikana kama ‘phytosanitary certificate’ kwa mujibu wa  Sheria inayosimamia ubora wa mazao (The Plant Protection Act 1997). Sheria hiyo inataka mazao yanayosafirishwa nje au kuingizwa nchini, yawe na ubora unaokubalika Kimataifa.
Bwana Mandepo alimalizia kwa kutoa wito kuwa nafasi ipo wazi kwa kila Mtanzania kuchangamkia fursa ya kusafirisha mazao nje ya nchi kwa kuwasilisha  maombi ya kibali kwa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kwa ajili ya kupata kibali hicho na kwamba Mfanyabiashara anayewasilisha maombi yake, anapaswa kuambatanisha leseni yake ya biashara, cheti cha mlipakodi na awe na idhini ya maandishi kutoka Wilaya au Mkoa ambako mazao husika yanatoka.

Changamoto za Pamba kupatiwa Ufumbuzi

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bwana  Zidikheri Mundeme amewataka wadau wa zao la pamba kuwalinda wakulima wadogo wa zao hilo kwa kuwapatia  pembejeo za kilimo kama mbegu bora na viuatilifu kwa wakati ili kuboresha zao hilo.

Bwana Mundeme alitoa wito huo, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa zao hilo kutoka nchini Kenya, Brazili na Tanzania, ambapo washiriki wa Tanzania walitoka katika Vituo vya Utafiti wa Mazao. Mkutano huo ulianza mapema wiki hii katika Hoteli ya Whitesands.

"Kilimo cha mkataba, ukosefu wa soko na uongezaji thamani wa zao hilo na kipato kidogo kwa wakulima wa zao hilo ni baadhi ya changamoto zinazomkabili mkulima mdogo wa pamba. Alieleza Bwana Mundeme

"Washiriki wa mkutano huo wanapaswa kujadili kwa kina namna ambavyo watatoa majibu ya changamoto hizo". Alikaririwa, Bwana Mundeme.

 

Serikali yasambaza vocha milioni 2.9 kwa Wakulima

Msemaji wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bwana Richard Kasuga amesema kiasi cha vocha 2,999,778 za pembejeo zenye thamani ya shilingi bilioni 78 zimesambazwa katika Mikoa 24 ya Tanzania Bara ili zitumike kufidia gharama ya mbolea na mbegu bora katika msimu wa kilimo wa mwaka 2015/2016.

Bwana Kasuga aliongeza kuwa wakulima zaidi ya 999,926 watanufaika na mpango huo na kuongeza kuwa vocha hizo zitajumuisha kiasi cha mbolea tani 99,993 huku kiasi cha 49,996 zikiwa ni mbolea ya kupandia na tani 49,996 zikiwa ni za kukuzia ambazo zote hizo zitapewa ruzuku ili kufidia sehemu ya gharama ya bei ya soko.

Bwana Kasuga aliongeza kuwa kiwango cha fidia hiyo ni  asilimia 50 ya bei ya soko kwa kila aina ya pembejeo inayopata ruzuku hiyo. Makampuni 23 ya mbolea na 27 ya mbegu bora yanaendelea kutoa huduma ya usambazaji wa pembejeo katika mikoa husika, na mkulima mnufaika atapatiwa pembejeo zinazotosheleza ekari moja ya mahindi na mpunga.

Aidha Bwana Kasuga ameeleza majukumu ya utekelezaji wa ruzuku ya pembejeo za vocha kuwa yamegawanyika katika ngazi sita ambazo ni; Wizara Kilimo Chakula na Ushirika, Kamati ya Taifa ya Uendeshaji wa Utaratibu wa Vocha, Mikoa, Wilaya, Kata na Vijiji.

Majukumu katika ngazi zote hizo ni pamoja na kutoa elimu ya usimamizi wa utekelezaji wa ruzuku ya pembejeo kwa wakulima, kutambua Kaya zinazonufaika, kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa mpango wa ruzuku kwa kutumia vocha na kuandaa taarifa za utekelezaji  na kuziwasilisha katika ngazi mbalimbali.

Pia amewataka wakulima kutorubuniwa na Mawakala wachache wasio waaminifu na kwamba mafaniko ya Sekta ya kilimo nchini yanamtegemea mkulima ambaye anatumia vizuri pembejeo kuongeza uzalishaji wa mazao husika. Aidha, kufanikisha mapinduzi ya kijani ni muhimu wakulima kutambua kwamba wanapoteuliwa kupewa vocha wanakuwa wamedhaminiwa na Taifa hivyo watumie dhamana waliyopewa kwa maslahi yao na ya Taifa kwa ujumla”. Alimalizia, Bwana Kasuga.

Serikali imeombwa kuwasaidia wasindikaji wa korosho

Washiriki wa Mkutano wa tatu wa Kimataifa wa korosho waliiomba Serikali kutoa msaada kwa wasindikaji wa korosho katika kufikia malengo.

Ombi hilo lilitolewa katika mkutano huo  uliofanyika katika Hotel ya Serena Jijini, Dar es Salaam.

Mkutano huo ni wa Kimataifa uliwakutanisha wadau wa zao la korosho kutoka nchi za Bara la Afrika, Ulaya na Asia.

Suala la Serikali kuwa na juhudi ya makusudi katika kuwasaidia wasindikaji wadogo na wa kati lilikuwa ni kilio cha wachangiaji mada walioshiriki mkutano huo.

Mchangiaji wa kwanza kupaza sauti yake alikuwa ni Waziri wa zamani katika Serikali ya Awamu ya Tatu, Bwana Maokola Majogo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Korosho, Mkulima na Msindikaji ambaye alisema kuwa kazi ya kuongeza thamani ya mazao katika Bara la Afrika ni ghali na kama wakulima wadogo na wa kati wakiachiwa kazi hiyo peke yao bila ya msaada wa Serikali ni dhahiri kuwa hawataweza, kuleta maendeleo ya zao la korosho.

Bwana Majogo aliongeza kuwa, ili mafanikio ya kweli yaweze kupatikana na kuonekana katika sekta ndogo ya korosho ni vyema maandalizi yaanze katika hatua ya uzalishaji (shambani) na hatmae usindikaji.

Bwana Majogo alikaririwa akisema “Hakuna namna ya kupata matokeo chanya; ni vyema uwekezaji ukaanzia kwenye maarifa ya uzalishaji na baadae kuwapatia wakulima, kipaumbele cha kuwasaidia fedha za mikopo nafuu ambayo, itawasaidia kununua mashine za kubangua, kupanga madaraja na kufungasha ili kuongeza thamani ya zao la korosho.”

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Bwana Mfaume Juma ambaye katika mkutano huo aliwasilisha mada inayohusu maendeleo ya sekta ndogo ya korosho nchini, alisema njia moja ya kuongeza uzalishaji katika zao la korosho ni kuhamasisha uwekezaji kwenye ujenzi wa viwanda vidogo na vya kati vya usindikaji wa mazao ya korosho.

 

Zidikheri Mundeme Ateuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Zidikheri Mgaya Mundeme  kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.

Bwana Mundeme anachukua nafasi ya Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Kabla ya uteuzi huo Bwana Mundeme alikuwa Wizara  ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Baada ya kufika Wizarani, Bwana Mundeme alifanya ziara ya kutembelea Idara na Vitengo kwa lengo la kufahamiana na watumishi na shughuli zinazotekelezwa katika maeneo yao ya kazi.

Katika ziara hiyo aliambatana na Eng. Raphael Daluti, Naibu Katibu Mkuu pamoja na  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu Bi. Hilda Kinanga.

 

 

 

 

Wekeza katika Kilimo Kuongeza Uzalishaji na Tija – Patrick Otto

Bwana Patrick Otto (kushoto) akifafanua jambo kwa Mheshimiwa Stephen Wasira (kulia) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani, Mkoa wa Simiyu.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) nchini Bwana Patrick Otto alisema njia pekee ya kupambana na umaskini ni kwa nchi Wanachama, duniani kote kuwekeza katika kilimo ili kuongeza tija na uzalishaji.
Takribani watu milioni 800 duniani kote, wengi wao wakiwa wanatoka Vijijini, hawana chakula cha kutosha na wanakabiliwa  na utapiamlo mkali huku zaidi ya watu bilioni moja wanaishi katika umaskini mkubwa.
Bwana Otto aliainisha juhudi ambazo FAO kwa kushirikiana na Serikali imekuwa ikifanyakatika kuendeleza kilimo nchini. Aliutaja Mpango wa Kuendeleza Kilimo unaojulikana kama Country Programming Framework – (CPF), chini ya Mpango huo, FAO  imeanza kusaidia katika eneo la kuendeleza kilimo cha biashara, maliasili na mazao yake na kuweka mipango endelevu katika kilimo na kuvutia uwekezaji.

Bwana Patrick alikaririwa akisema “Siku ya Chakula Duniani mwaka huu iwe ni fursa ya kutafakari juu ya malengo huku nchi 193 zimekubaliana na ajenda mpya ya maendeleo  endelevu hususan kukomesha njaa duniani kote ifikapo mwaka 2030”.

Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani mwaka huu, yalikwenda sambamba na tukio la upandaji miti 70 ya matunda katika Viwanja vya Shule ya Somanda A na B.
Shughuli hiyo ilifanywa kwa ushirikiano wa uongozi wa Mkoa wa Simiyu, Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi lengo likiwa kuweka kumbukumbu ya miaka 70 ya FAO.
Huu ni mwaka wa 35 tangu dunia ianze kuadhimisha, Siku ya chakula duniani ambayo hufanyika ifikapo tarehe 16/10 kila mwaka. Maadhimisho ya mwaka huu yanaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 70 ya FAO. Kaulimbiu ya maadhimisho ya Siku ya Chakula kwa mwaka huu inasema; Kilimo na Hifadhi ya Jamii katika kuondoa Umaskini Vijijini.

 

 

Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani Yafana

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mheshimiwa Stephen Masatu Wasira (mwenye suti nyeusi) akikagua mabanda katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani Bariadi – Mkoa wa Simiyu

Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Chakula Duniani yalifikia kilele chake tarehe 16 Oktoba 2015 katika kiwanja cha halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Mheshimiwa Stephen Masatu Wasira.  Maadhimisho hayo yalipambwa na maonyesho na burudani mbalimbali za kwaya na vikundi vya ngoma vikiwa vimebeba ujumbe wa siku ya chakula duniani. Katika maadhimisho hayo, Mheshimiwa Wasira alitembelea na kukagua mabanda ya maonyesho ya bidhaa za kilimo, ufugaji na  uvuvi yaliyokuwa yakionyeshwa na wataalamu na wajasiliamali kutoka taasisi za umma na wadau mbalimbali.

Maadhimisho hayo kwa mwaka huu yalibeba kaulimbiu inayosema “Kilimo na Hifadhi ya Jamii katika Kuondoa Umaskini vijinini.”

Katika hotuba ya kilele cha maadhimisho hayo, Mheshimiwa Wasira alisema kuwa kaulimbiu hiyo inatukumbusha kuwa Serikali inao wajibu wa kutunga Sera na kuandaa program zinazozingatia kutatua matatizo ya kiuchumi, kimazingira na kijamii ili kuondoa uhaba wa chakula na umaskini vijijini.

Akinukuu takwimu zinazotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), mheshimiwa Wasira alisema kuwa, kupitia mipango thabiti ya hifadhi ya jamii, takribani watu milioni 150 duniani kote wamesaidiwa kuondokana na umaskini.

 Alisema kuwa zaidi ya watu milioni 870 duniani kote, mtu mmoja kati ya watu tisa anaishi kwenye njaa ya kiwango cha juu, huku asilimia 60 ya idadi hiyo ya watu wakiwa ni wanawake na zaidi ya watoto milioni 5 duniani kote wako katika hatari ya kufariki kutokana na utapiamlo.

Akizungumzia hali ya chakula nchini Tanzania, Waziri Wasira alisema kuwa, Serikali imeendelea kufanya juhudi kubwa ya kuwasaidia wakulima wadogo, wafugaji na wavuvi ili waweze kujiletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kujipatia chakula cha kutosha na lishe bora. Aliendelea kusema  kuwa katika Serikali ya Awamu ya Nne kumekuwa na mikakati na programu mbalimbali ambazo zimetekelezwa na kuchangia kikamilifu katika kukuza kilimo na hifadhi ya jamii.   Alitaja programu na mikakati ambayo ni:- Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDS) wa mwaka 2002; na Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP) ya mwaka 2006.

 

 

Wakulima Laki 5 Wapatiwa Mafunzo na Mradi wa EAAPP

Afisa Kilimo Mkuu Bi. Justa Katunzi akitoa maelezo ya mafanikio ya Mradi wa EAAPP ofisini kwake 

Wakulima 599,290 kutoka Wilaya 48 hapa nchini, wamepatiwa mafunzo ya kilimo bora na mbinu za ujasiriamali katika kilimo kupitia Mradi wa EAAPP ulionza kutekelezwa mwaka 2010 hadi sasa. Hayo yamebainishwa na Afisa Kilimo Mkuu Bi. Justa Katunzi alipoongea na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ofisini kwake. Aliongeza kuwa wakulima wawezeshaji 2,414 na Maafisa Ugani, wapatao 697 nao walipatiwa mafunzo ili wasaidie wakulima katika maeneo wanayotoka.

Mafunzo hayo yalihusisha matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo kama mbolea, mbegu bora na matumizi ya madawa ya kuua wadudu, mafunzo hayo yalikuwa yakitolewa kwa njia ya mfumo wa shamba darasa ambapo wakulima wawezeshaji na wataalam wanafundisha wakulima kwa vitendo.

Mafunzo hayo yamewafanya  wakulima kuzingatia kanuni za kilimo cha kisasa hali ambayo imechangia matumizi ya mbegu bora kufikia  asilimia 90 katika maeneo yaliyofikiwa na mradi wa EAAPP. 
.
Aidha, Bi. Katunzi aliongeza kuwa mafunzo hayo yamewezesha wakulima kutoka Wilaya za Mbarali, Kilombero na Mvomero wanaotumia kilimo cha umwagiliaji kuongeza uzalishaji kutoka tani 2.5 na kufikia tani 8 kwa hekta na Wilaya ya Ukerewe inayotegemea mvua katika kilimo cha mpunga mavuno yamefikia 3.4 kutoka 1.5 kwa hekta.“Mafunzo ya ujasiriamali katika kilimo  yanayotolewa kupitia Mradi wa EAAPP yamewezesha wakulima kuongeza kipato kwa kuepuka hasara walizokuwa wakipata kutoka kwa walanguzi waliokuwa wakitumia vipimo visivyo rasmi kama vile lumbesa kuwadhulumu wakulima” Bi. Katunzi alifahamisha katika mazungumzo yake.

Alibainisha pia kuwa kabla ya mafunzo hayo, wakulima walikuwa wakiibiwa mazao yao kwa kutumia rumbesa, walikuwa wakiuza kilo 120  za mpunga kwa sh. 70,000 wakati kipimo halali ni kilo 100. Mafunzo hayo ya ujasiriamali, yamewawezesha wakulima kujua gharama walizotumia toka kuandaa mashamba,  kupanda na kuvuna hali ambayo imewawezesha kupanga bei ya kuuzia mazao kulingana na gharama za uzalishaji na bei ya soko. Mradi wa EAAPP ulianza  kutekelezwa mwaka 2010 na utakamilika mwezi Desemba, 2015.

 

 

Tathmini ya Mashine za Kuvunia Mpunga Yafanyika

 

Wataalamu 20 kutoka Idara ya Zana za Kilimo  wameanza kufanya tathmini ya mashine mbalimbali za kuvunia mpunga kufuatia mafunzo yaliyotolewa awali juu ya matumizi na uendeshaji lengo likiwa ni kutatua vikwazo vilivyojitokeza wakati wa matumizi na uendeshaji wake. Hayo yalibainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Zana za Kilimo Eng. Rajabu Mtunze alipozungumza  na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali ofisini kwake, hivi karibuni.

Wilaya zinazofanyiwa tathmini na  wataalam hao wa zana za kilimo ni Mbarali Mkoa wa Mbeya, Songea, Mkoa wa Ruvuma;  Mvomelo na Kilosa katika Mkoa wa Morogoro. Eng.  Mtunze alizitaja Wilaya nyingine kuwa ni Iringa Vijijini, Mkoa wa Iringa; Bagamoyo Mkoa wa Pwani na Korogwe Mkoa wa Tanga.

Wilaya zilizopata mafunzo hayo kwa Mkoa wa Kilimanjaro ni Mwanga na Hai wakati katika Mkoa wa  Arusha ni Arumeru na Babati katika Mkoa wa Manyara.

Mashine zitakazofanyiwa tathmini ni ‘Combine Harvester’ ambazo zina uwezo wa kuvuna, kukoboa na kufungasha mpunga katika mifuko. Mashine nyingine ni za kupandia ‘Leaper”. Mashine nyingine ni za kukata na kupiga punga ‘Thresher’.

 “Wataalamu hao pia watatoa mafunzo kwa waendeshaji wapya wa mashine hizo baada ya wengine kumaliza mikataba yao na pia watafuatilia ujenzi wa majengo ya kuwekea mashine za kukoboa na kupanga madaraja ya mpunga kuhakikisha yanakamilika ili mashine hizo zianze kufanya kazi”, alibainisha Eng. Ntunze.

 

 

Wafanyabiashara Washiriki katika Kilimo – Komba

Mratibu wa Sera ya  Afya ya Udongo ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Pembejeo toka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bw. Canuth Komba ameitika sekta binafsi hapa nchini kushiriki kikamilifu katika kuinua kilimo.
 
Komba alitoa wito huu wakati wa mkutano wa Sera ya Afya ya Udongo  uliofanyika katika Hoteli ya LandMark Jijini Dar es Salaam, alisisitiza kuwa muda umefika kwa sekta binafsi kujikita kikamilifu katika kuboresha kilimo kwa manufaa ya wakulima wetu.

“ Serikali peke yake haiwezi kuinua kilimo chetu bila ushiriki wa sekta binafsi  kikamilifu na hasa kwa wafanyabiashara wetu ambao ni nguzo muhimu katika uhakika wa soko la mazao ya wakulima.” alisisitiza Bw. Komba.

Wafanyabiashara ni watu muhimu sana katika kulisukuma gurudumu la kuinua sekta ya kili mo, aliongeza Komba.

Pia alifahamisha kuwa utafiti  umefanyika kwa lengo la kuwashauri watunga sera wetu kuwa na sera ya matumizi bora na sahihi ya mbolea kwa wakulima.

Elimu kwa wadau wa kilimo juu ya matumizi sahihi ya mbolea ni muhimu sana katika kufikia lengo kubwa la kuongeza uzalishaji wa kilimo chetu.

Mkutano huo wa siku moja  pia uliwashirikisha wadau mbali mbali kutoka Wizara Kilimo Chakula na Ushirika, Sekta Binafsi, Wakulima, Wafanyabiashara, watalaamu toka chuo kikuu cha Sokoine na chuo kikuu cha Mzumbe na nje ya nchi.

Mada mbali mbali ziliwasilishwa katika mkutano huo zikiwa na lengo la kuendeleza kilimo  kwa maslahi ya wakulima na taifa kwa ujumla katika harakati za kuondoa umasikini miongoni mwa Watanzania na kukuza pato la taifa.

 

Wabia wa Maendeleo watia sahini kuisaidia SAGCOT

Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Bibi Sophia Kaduma akitia sahini utekelezaji wa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Wabia wa Maendeleo ili kusukuma kwa pamoja malengo ya SAGCOT, kushoto kwake ni Bibi, Hanne- Marie Kaarstad, Msimamizi Mkuu wa maendeleo kutoka Ubalozi wa Norway na anayefuatia ni Bwana Eric Beaume, kutoka Idara ya Mahusiano ya Jumuia ya Ulaya.

 
Wabia wa Maendeleo wakiongozwa na Bwana Philippe Dongier, Mkurugenzi Mkazi wa Bank ya Dunia nchini, leo wametia sahini ya makubaliano ya kuisaidia SAGCOT, makubaliano hayo ni utekelezaji wa ahadi za wabia hao ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Mpango huo.
SAGCOT ni kifupi cha maneno, chenye maana ya Southern Agricultural Growth Corridor Growth of Tanzania tafsiri yake ni Mpango wa Kuboresha Kilimo Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini ilianzishwa miaka mitatu iliyopita leo lake kubwa na kusaidi uwekezaji mkubwa na mdogo katika kilimo kwa kushirikiana na sekta binafsi.
Awali katika hotuba yake ya ufunguzi wa tukio hilo, Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Bibi Sophia Kaduma alisema kutiliana sahini ni mwanzo mzuri, kwani Serikali kwa kushirikia na sekta binafsi, maendeleo katika sekta ya kilimo yatafikiwa kwa haraka.
Bibi Kaduma alisema, lengo la Serikali ni kupunguza umaskini, kuboresha maisha ya watu vijijini na mijini na kuongeza kuwa kiasi cha dola bilioni 2.1 za Marekani ambazo zitawekezwa kupitia Mpango huo zitachangia katika ukuaji wa uchumi kupitia kilimo.
Naye Bwana Vel Gnanendran, Mwakilishi wa Mkazi wa DFID alisema huu ni mwanzo mzuri na tukio la kutiliana sahini ni mwanzo mzuri na kwamba wabia wa maendeleo wapo mstali wa mbele kuhakikisha, malengo ya SAGCOT yanafikiwa ikiwa ni pamoja na kuboresha utendaji kazi wa Mpango huo.
Bwana Geoffrey Kirenga, ambaye ndiye Mtendaji Mkuu wa SAGCOT alisema, Mpango huo unatekelezwa kwa pamoja kati Serikali kwa kushirikiana na wabia wa maendeleo na kuishukuru Serikali kwa kuja na mtazamo mpya wa kuishirikisha Sekta binafsi katika kukuza na kuendeleza uchumi wa Taifa.
Bwana Kirenga aliongeza kuwa, sasa ni wakati wa kila Mtanzania kubadili fikra kwa kuwa, maendeleo yanaletwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi, na kushauri Watanzania kuacha fikra za kusubiri kusaidiwa.
Bwana Kirenga alisema mpaka sasa, wabia wa maendeleo wametoa ahadi ya kiasi cha Dola za Kimarekani, bilioni 1 ambazo zitatolewa punde ili kuanza utekelezaji katika eneo la usimamizi na uratibu wa shughuli za SAGCOT.

 

 

WAZIRI AFANYA ZIARA MKOANI MBEYA

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika amefanya ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Mbeya kukagua shughuli mbalimbali za kilimo mkoani humo, akiwa wilayani mbarali waziri aliwataka watendaji wa Halmashauri kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN).Vilevile ameagiza kuundwa kwa timu ya wataalamu kuchunguza sababu za kubomoka bwawa la lwanyo lilopo katika kata ya Igurusi wilayani mbalali.
Akiwa wilayaniMomba aliwataka wanakijiji wa kijiji cha Ukwile kata ya Isandula kutumia fulsa ya mipaka ya nchi za jirani kama Malawi na Zambia katika kupata masoko ya mazao yao pia Halmashauli na sekta binafsi kutatua changamoto za fedha zinazowakabili.
Waziri akiwa wilayani Mbozi alikagua maendeleo ya ununuzi wa mahindi unaofanywa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Wilayani humo.

 

 

Zambi : Wahujumu wa Ushirika Kukiona

Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mheshimiwa Godfrey Zambi akipata maelezo toka kwa viongozi wa wilaya ya Mvomero

Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mheshimiwa Godfrey Zambi amesema serikali itachukua hatua kali kwa watu wote watakaohusika na kuhujumu vyama vya ushirika hapa nchini.
Mheshimiwa Zambi aliyasema hayo wakati akitoa salamu zake katika ziara ya Waziri wa Kilimo Chakula na Ushrika Mheshimiwa Eng. Christopher Chiza mkoani Morogoro.
“ Viongozi wa vyama vya ushirika ndio tatizo Kubra katika ustawi wa ushirika hapa nchini kwani wamekuwa chanzo cha kuhujumu ushirika” aliongeza Mhe. Zambi.
Wamekuwa wakitumia nafasi zao za uongozi kwa kujipendelea katika utoaji wa mikopo,  alisisitiza Mheshimiwa Zambi katika hotuba yake.
“ Tumetunga sheria namba 6 ya Ushirika ya mwaka 2013 itakayowabana viongozi hawa wa ushirika wanaokwenda kinyume na uendeshaji wa ushirika” alifahamisha Mheshimiwa Zambi.
Sheria hii ni kali sana na itawabana kikamilifu wanaohujumu ushirika  na hivyo kurudisha nyuma nia ya wananchi kuwa na maisha bora, aliongeza.
Alisema  tatizo lingine linalokwamisha na kuathiri ushirika ni utitiri wa vyama vya ushirika katika sehemu moja.
Kuna vyama vya ushirika ambavyo havifanyi kazi iapasavyo katika kuendeleza ushirika wetu bali vinakuwepo kwa jina tu.
“ Kuna umuhimu  kuwa na vyama vichache vyenye ufanisi kuliko ilivyo sasa ambapo kuna mlundikano vyama usio na tija kwa wanaushirika” alifahamisha Mhemiwa Zambi.

 

 

KILIMO CHA UMWAGILIAJI KUCHANGIA ASILIMIA 25 YA CHAKULA

 

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Mheshimiwa Eng.  Christopher Kajoro Chiza (Mb) ameeleza  kuwa, kilimo cha umwagiliaji  kina nafasi ya kuchangia asilimia 25 ya chakula  kinachozalishwa nchini.  Aliyalisema hayo wakati  alipotembelea mradi wa umwagiliaji wa Nkoanrua katika Halmashauri ya  Wilaya ya  Meru.
Azma hiyo inaweza kufikiwa kwa  kuongeza eneo,   pamoja na kuongeza tija katika maeneo yaliyopo. Hatua za kuchukua ni pamoja na kubadili kilimo cha kujikimu kuwa cha kibiashara.
Alisisitiza kuwa hatua hiyo itafikiwa endapo wakulima watabadilika na  kulima kilimo cha kisasa badala ya  kilimo cha mazoea.
Hatua nyingine ni kukarabati na kuisafisha mifereji  ya umwagiliaji iliyopo kwa lengo la kupunguza upotevu wa maji ili kuleta ufanisi katika matumizi ya maji.  Vile vile aliwahimiza wakulima kuzalisha mara mbili katika msimu, aliongeza Mheshimiwa Chiza.
Aidha, alihimiza umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji na kuwa na Kamati ya watumia maji ili kuboresha huduma za umwagiliaji.
Hatua hizo zitawezesha kufikiwa kwa malengo ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambapo ifikapo  mwaka 2015 kuwe  na ongezeko la mavuno  kwa  zao la mahindi la tani 100,000, mchele tani 290,000 na Sukari tani 150,000.

 

 

WIZARA YAENDESHA MAFUNZO

Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika imeendesha  mafunzo ya usimamizi na uhifadhi wa zao la mpunga baada ya mavuno,  yaliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Edema katika Manispaa Morogoro kuanzia tarehe 20 – 31 Januari, 2014.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Idara ya Zana  Eng. Mark Lyimo, Mafunzo hayo yaliwwahusisha Maafisa Zana na Ugani wapatao 14 na wakulima 84 kutoka skimu 14 za umwagiliaji wa Halmashauri za Mikoa ya Mbeya, Morogoro, Tanga, Arusha, Iringa, Kilimanjaro Manyara na Ruvuma.
Pia katika mafunzo haya taasisi binafsi ya RUDI ilishiriki ikiwa ni katika harakati za  kushirikisha  sekta binafsi katika kuboresha kiilimo hapa nchini.
Baadhi ya mada zilizowasilishwa katika mafunzo haya ni pamoja na  uzalishaji kitaalam,  usindikaji wa zao la mpunga na kanuni zake, Uhifadhi bora wa zao la mpunga, ufungashaji na kupiga chapa bidhaa za mpunga katika kulenga soko, alifafanua Eng. Lyimo.
“Lengo kubwa la mafunzo haya ni kutoa elimu kwa maafisa zana na wakulima kwenye skimu za umwagiliaji ili waweze kutumia teknolojia za kisasa katika kuzalisha, kuvuna na kuhifadhi katika kuongeza thamani kwa lengo la  kuboresha na kuongeza tija kwa mkulima mdogo katika maeneo ya umwagiliaji hapa nchini” aliongeza Eng. Lyimo.
Mada  nyingine ni kanuni bora za uzalishaji wa zao la mpunga, usindikaji,  matumizi sahihi ya mashine  bora katika kilimo cha mpunga zitakazotolewa na Serikali katika skimu 14 chini ya Mradi wa Sera na Maendeleo ya Rasilimali Watu (PHRD), alifafanua Eng.  Lyimo.
Mafunzo haya ni sehemu ya utakelezaji wa mpango wa  Serikali wa Matokeo Makubwa  Sasa (BRN) kwa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika ambapo zao la mpunga  ni mojawapo linalopewa kipaumbele katika kuongeza uzalishaji na tija.

 

 

Taasisi za Wizara ya Kilimo zatakiwa Kupunguza na Utegemezi

Wakuu wa Taasisi za Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika walipokutana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Sophia Kaduma hivi karibuni katika ukumbi wa Kilimo I

Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika zimetakiwa kuwa na mikakati ambayo itaziwezesha kujitegemea katika  shughuli zao  ili kupunguza utegemezi katika mfuko wa serikali.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wizara ya kilimo chakula na ushirika Bibi Sophia Kaduma katika Kikao  kilichojumuisha Wakuu wa taasisi hizo  kilichofanyika katika ukumbi wa Kilimo I hivi karibuni
Akiwasilisha taarifa yake Bibi Sophia amezitaka kila Taasisi kuainisha vyanzo vyake vya mapato   nje ya ruzuku  ya serikali  ikiwemo michango ya wadau . ‘kila Taasisi kwa namna moja au nyingine inakusanya mapato yake, “nataka kila mkuu wa Taasisi aainishe  vyanzo vyake vya fedha anavyotegema kukusanya katika mwaka 2014/15” alisema Bibi Kaduma.
Aidha katika kikao hicho wakuu wa taasisi walipata fursa ya kubadilishana uzoefu wa namna bora ya kuendesha taasisi hizo pamoja na ubunifu wa kujipatia fedha kutokana na rasilimali zake.  
Pamoja na hayo Katibu Mkuu alisisitiza kuwa vikao vya namna hiyo vitakuwa vinafanyika angalau kila robo mwaka ili kuongeza ufanisi katika kusimamia taasisi hizo.

 

 

WAZIRI WA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA AMESEMA HAPENDI KUONA TASNIA YA SUKARI IKIKOSA MWELEKEO

"Mhe. Eng. Christopher Kajoro Chiza Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika akitoa hotuba kwa Wadau wa Sukari katika Mkutano uliofanyika Mjini Morogoro Mwanzoni mwa Januari 2014.

 

Mhe. Eng. Christopher Kajoro Chiza (Mb) Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika ameonya kuwa kuwa Serikali haitapenda kuona Tasinia ya Sukari ikikosa mweleleo kutokana na matakwa ya kundi fulani. Alisisitiza kuwa, Tasnia ya sukari ni moja ya tasnia kubwa nchini ikijumuisha wadau muhimu wakiwamo walaji, wakulima, wafanyabiashara na wazalishaji. Kila mdau katika jumuisho hili ana maslahi ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kukinzana na ya mdau mwenzake. Mkulima angependa kuona anauza miwa yake kwa bei ya juu, hali kadhalika mzalishaji kuuza sukari anayozalisha kwa bei yenye faida ya kutosha. Aidha mfanyabiashara angependa kupata faida maradufu na panapokuwa na mwanya kuingiza sukari kutoka nje kwa njia sizizo halali. Lakini kwa upande mwingine mlaji naye angependa kununua sukari kwa bei nafuu.

Serikali haipo tayari kuona tasnia kubwa na muhimu kama hii ya sukari ikipoteza mwelekeo, aidha ingependa kuwepo kwa mazingira mazuri (win - win situation) kwa kila mdau. Kwa maana hiyo nimeona ni jambo jema na muhimu sana kuwakutanisha ninyi wadau ili tuweze kujadili kwa pamoja changamoto zilizopo mbele yetu juu ya sekta hii. Ni matarajio yangu kwamba, mkutano huu utaweka misingi ya kufikia utatuzi wa chamngamoto hizi kwa manufaa ya pande zote

Mhe. Waziri ameyasema hayo katika mkutano wa Wadau wa Sukari uliofanyika Mjini Morogoro mwanzoni wa mwezi Januari

Akitoa picha halisi ya uzalishaji na mahitaji ya sukari hapa nchini Waziri Chiza alisema kuwa, Wakati viwanda vyetu vinabinafsishwa vilikuwa vinazalisha wastani wa tani 120,000 kwa mwaka. Sasa uzalishaji umefikia wastani wa tani 300,000 kwa mwaka.

Aidha uzalishaji wa miwa (siyo sukari) katika mashamba ya wakulima wadogo nao umeongezeka kwa asilimia 61 (hii ni kutoka wastani wa uzalishaji wa tani 439,122 hadi tani 705,176 kwa mwaka). Uzalishaji katika mashamba ya wenye viwanda umeongezeka kutoka wastani wa tani 1,083,738 na kufikia tani 2,229,274 kwa mwaka (ongezeko la asilimia 105).

Pamoja na mafanikio haya bado tasnia ya sukari imegubikwa na changamoto mbali mbali kubwa zaidi ikiwa uzalishaji usiokidhi mahitaji. Mahitaji yetu ni wastani wa tani 590,000 za sukari kwa matumizi ya kawaida na ya viwandani. Viwanda vya sukari nchini huzalisha takribani asilimia sabini tano (75%) ya mahitaji ya sukari ya matumizi ya kawaida. Wastani wa tani 290,000 ni nakisi inayojazwa na uagizaji sukari kutoka nje. Nakisi hii inajumuisha sukari ya matumizi ya kawaida (gap sugar) ya wastani wa tani 120,000 na sukari ya matumizi ya viwandani ya wastani wa tani 170,000 kwa mwaka. Kiasi chote cha sukari ya matumizi ya viwandani kinaingizwa nchini kutoka nje. Aidha uagizaji wa sukari ya matumizi ya kawaida unategemea hali halisi ya soko kwa kipindi husika na kwa hiyo uagizaji halisi unaweza kuwa juu au chini ya nakisi hiyo. Hata hivyo, Kamati ya Ufundi ya Ushauri ya Uagizaji Sukari iliyokutana tarehe 24/12/2013 kujadili hali ya sukari nchini imependekeza kuwa mwaka huu 2013/2014 kusiwe na uagizaji wa sukari kwa sababu kiasi tha tani 257,000 kitapatikana kwa matumizi ya kawaida kuanzia sasa hadi mwishoni mwa 2013/2014.

 

ZIARA YA WAZIRI MTWARA

Mhe. Eng. Christopher K. Chiza (MB) Waziri wa Kilimo Chakula na ushirika akikagua ujenzi wa ghala la TANECU (Tandahimba Newala Cooperative Union) Ghala hilo litakuwa na uweza wa kuhifadhi tani 10,000 za korosho na linajengwa Tandahimba . Ghala hilo ni maandalizi ya ujenzi wa kiwanda cha kubangulia korosho kitakachojengwa na TANECU.

 

Mhe. Eng. Christopher K. Chiza (MB) Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, akipata maelezo ya zana inayotumika kuandaa mashamba ya mpungaa katika kijiji cha Mahuninga wilaya ya mtwara. Mashamba hayo yenye ukubwa wa ekari 1,000 yanalimwa na mwekezaji mzalendo Bw. Hamis Ismail Msigwa ambaye anashirikiana na vijiji vya Mahuninga na kitunguli.

 

Mhe. Eng Christopher K. Chiza (MB) akikagua shamba linaloandaliwa kwa ajili ya kilimo cha mpunga katika kijiji cha Mahuninga katka Wilaya ya Mtwara. Mashamba hayo yanamilikiwa na mwekezaji mzalendo Hamis Ismail Msigwa.

 

The future is bright for Farmers in Tanzania – Crop Production to Increase through 2KR Fund  

Eng. Christopher Kajoro Chiza, the Minister for Agriculture Food Security and Cooperatives shaking hand with Mr. Masaki Okada, the Ambassador of Japan in Tanzania after receiving 6,003.6 tons of fertilizer which value Tanzanian Shillings 7.3 billion .S

The Government of Japan has donated 6,003.6 tons of DAP fertilizer worth Tanzanian Shillings 7.3 billion to the Government of Tanzania. This assistance is coming when the country is determined to turn around Tanzanian agriculture through intensification which entails use of inputs such as fertilizers and improved seeds.
This assistance comes as good news to Tanzanian small scale farmers that the mineral fertilizer received under this bilateral arrangement between the two countries will contribute to the efforts of eliminating some of the challenges to bring about food crop production and productivity in the country.
 Speaking at the handover ceremony, Eng. Christopher Kajoro Chiza, the Minister for Agriculture Food Security and Cooperatives, said that, the Tanzanian farmers face several challenges.
“Small holder food crop production and productivity in Tanzania has remained low due to many challenges facing agricultural development in the country; these challenges include inaccessibility to agricultural inputs” the Minister said.
Through additional use of fertilizers, Tanzania can immensely increase crop production particularly cereals such as rice, maize and sorghum. These crops are important staples dependent upon to meet the domestic food requirements and production of surplus for export in the East and Central African region.
Current data show that cereals production in Tanzania reached 6.8 million tons in 2012 cropping season which fall short of the national demand of 7.2 million tons. The deficit of 0.4 million tons of cereals can be offset by additional use of inputs such as fertilizers coupled with other agronomic packages.
Mr. Masaki Okada, the Ambassador of Japan in Tanzania, who was present at the hand-over ceremony, said that, the Government of Japan is in the forefront to support the efforts of the Government of Tanzania to increase food production and productivity.
He further said that, Aid for the Increase of Food Production –popularly known as KR II program, which started way back in 1978, has assisted Tanzania to address some of the agricultural challenges.
“Since 2010, when the KR II program was reviewed to be known as Grant assistance for food security project for underprivileged farmers (or 2KR) also provided 5,953 tons of DAP  fertilizers in 2011”, said Mr. Masaki Okada.         
 The Government of Japan also supports Tanzania agricultural development initiatives such as Agricultural Sector Development Program (ASDP), and the development of the National Rice Development Strategy for increasing rice production and productivity in the country.
The Minister, Eng. Chiza, thanked the Government of Japan for being so committed in the development agenda of Tanzanians. In a note of appreciation, the Minister Chiza said,
“we envisage that the Government of Japan will still be willing to support Tanzania in the implementation of the Rice Development Strategy in – developing improved high yielding varieties; development of improved post harvest processing technologies; value addition processes; labour saving technologies and construction of more irrigation infrastructures. This areas will certainly enable us to achieve the Big Result Now initiatives”.
Highlighting the impacts of past assistance from Japan under KR II, Minister Chiza said that, between 1992 and 2010, over 24.3 billion shillings was received from the sales of commodities received from Japan. The funds were used to finance over 186 development projects in Tanzania. These projects include those that have wider social economic impact such as agriculture, education, health, feeder roads and domestic water supply.
The funds to be generated from the sale of the DAP fertilizer will else well be used to finance social economic development projects particularly those focusing the underprivileged farmers to improve agricultural production, farm to market infrastructures and domestic water supply. These areas are those agreed upon by the two governments.

 

 

Farmers in Eastern Africa region Hopeful to Increase Rice Production

Tanzania is hosting the First Regional Rice Review and Planning Meeting that is taking place from 30th September to 4th October 2013 at Peacock Hotel in Dar es Salaam, Tanzania. 
The meeting opening ceremony was graced by the Deputy Permanent Secretary Ministry of Agriculture Food Security and Cooperatives of Tanzania Dr. Yamungu Kayandabila.  
Over 100 participants mostly scientists from four countries – Ethiopia, Kenya, Tanzania and Uganda which are implementing the Eastern Africa Agricultural Productivity Project (EAAPP) attended the meeting.
The meeting objectives fall within the general mandate of EAAPP which is in line with the African Union/ NEPAD’s strategy for agricultural growth, the Comprehensive Africa Agricultural Program (CAADP) which is that of increasing agricultural productivity in Pillar IV framework.
Dr. Kayandabila, in his opening statement, commended the regionality aspect in fostering collaborations in tackling agricultural development challenges.
He said that “Globalization presents many challenges to our regional and as such cooperating with each other with the aim of achieving mutual benefits in terms of technology development is indeed very crucial”.
He further said that, “EAAPP approach has continued to develop and work through highly specialized state of the art and high level Centres’ of Excellency which are expected to be hubs of knowledge, technology and information of the four commodities among which is the Regional Rice Centre of Excellence”.  
The meeting is important for the Eastern Africa Countries particularly Tanzania’s economy where rice is the  second most important crop after maize and one of the major cash crop. In Tanzania rice is predominantly grown by small scale farmers under rain fed lowland, upland and irrigated ecosystems.
The annual demand of rice in Tanzania has been increasing as a result of population increase, expansion of urbanization and dietary shift from other conventional food.
On the other hand, it is also interesting to mention that rice production in Tanzania has more than doubled from 1,162,690 tons in 2005 to 2,650,120 tons in 2011.
This increase in production is attributed to the increase in acreage from 701,990 hectares to 1,319,320 hectares in the same period. Another attributes to the increase in production of rice in Tanzania among others include use of new improved rice varieties such as SARO 5 (TXD 306) and TXD 85.
Other attributes are provision of fertilizer subsidies by the Government of Tanzania which has brought about increase in fertilizer use by small scale farmers.
Tanzania is hosting the First Regional Rice Review and Planning Meeting that is taking place from 30th September to 4thOctober 2013 at Peacock Hotel in Dar es Salaam, Tanzania.
The opening ceremony of the meeting was graced by the Deputy Permanent Secretary, Ministry of Agriculture Food Security and Cooperatives, Dr. Yamungu Kayandabila.
Over 100 participants mostly scientists from four countries– Ethiopia, Kenya, Tanzania and Uganda which are implementing the Eastern Africa Agricultural Productivity Project (EAAPP) are attending the meeting.
The meeting objectives fall within the general mandate of EAAPP which is in line with the African Union/ NEPAD’s strategy for agricultural growth, the Comprehensive Africa Agricultural Program (CAADP) which is that of increasing agricultural productivity in Pillar IV framework.
Dr. Kayandabila, in his opening statement, commended the regionality aspect in fostering collaborations in tackling agricultural development challenges.
He said that “Globalization presents many challenges to our regional and as such cooperating with each other with the aim of achieving mutual benefits in terms of technology development is indeed very crucial”.
He further said that, “EAAPP approach has continued to develop and work through highly specialized state of the art and high level Centres’of Excellency which are expected to be hubs of knowledge, technology and information of the four commodities among which is the Regional Rice Centre of Excellence”.
The meeting is important for the Eastern Africa Countries particularly Tanzania’s economy where rice is the second most important crop after maize and one of the major cash crop. In Tanzania rice is predominantly grown by small scale farmers under rain fed lowland, upland and irrigated ecosystems.
The annual demand of rice in Tanzania has been increasing as a result of population increase, expansion of urbanization and dietary shift from other conventional food types.
On the other hand, it is also interesting to mention that rice production in Tanzania has more than doubled from 1,162,690 tons in 2005 to 2,650,120 tons in 2011.
This increase in production is attributed to the increase in acreage from 701,990 hectares to 1,319,320 hectares in the same period. Another attributes to the increase in production of rice in Tanzania among others include use of new improved rice varieties such as SARO 5 (TXD 306) and TXD 85.
Other attributes are provision of fertilizer subsidies by the Government of Tanzania which has brought about increase in fertilizer use by small scale farmers.
Over the current years, rice is among important export crop which has equally promoted production of the crop in the region.
Tanzania is home to the Regional Rice Center of Excellence (RRoCE) which is located in Ifakara, Morogoro region in Eastern Tanzania. Despite RRoCE being situated in Tanzania but scientists from across the four countries are doing research to generate technologies to enhance production and utilization of rice along the value chain.
In this regional rice review and planning meeting scientists have the opportunity to present their work, share experiences and discuss future project proposals.
It is anticipated that this meeting fulfills the pre-set goal of EAAPP which is:
“to contribute to enhanced sustainable productivity, value added and competitiveness of the sub-regional agricultural system”
Furthermore, this meeting has been organized to challenge scientists to stay focused towards achieving the specific objectives of EAAPP which are to:

  • Enhance regional specialization in agricultural research
  • Increase regional collaboration in agricultural training and dissemination
  • Facilitate increased sharing of agricultural information, knowledge and technology across national boundaries

The rice farmers in the four countries where EAAPP is being implemented are looking forwards to the outcomes of this meeting and others to come, not only for meeting the objectives and goals of the project, but of most interest to them is to get technologies which can enable them to produce more rice efficiently which will provide more on the table.
It is therefore in the interest of farmers and other stakeholders in the Eastern Africa region that the rice sub-sector will make a difference in improving livelihood and economies of the region though these established research collaborations under EAAPP.

 

 
 

Tanzania na Afrika ya Kusini Kushirikiana Katika kilimo

Timu kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirka na timu kutoka wizara ya mifugo zote za Tanzania na timu kutoka wizara ya kilimo ya Afrika ya kusini

Wizara ya Kilimo  Chakula  na Ushirika ya Tanzania imekutana na wizara ya kilimo ya Afrika ya kusini hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Kilimo I  lengo likiwa ni kujadiliana maeneo ambayo serikali hizi mbili zinaweza kushirikiana katika sekta ya kilimo.
Katika mkutano huo  ulibainisha kwamba ili kukuza sekta ya kilimo na kilimo kuweza kuleta manufaa kwa wakulima wengi katika nchi hizi mbili ni lazima kuwekeza katika utafiti na matumizi ya zana bora za kilimo.
Akiongea katika mkutano huo Mratibu wa Mashirikiano na Misaada ya Kimataifa Bi Magreth Ndaba alisema kwamba lengo la mashirikiano hayo ni kuimarisha usalama wa chakula, kubadilishana teknolojia za uzalishaji wa mbegu za kisasa, kuimarisha sekta za umwagiliaji  pamoja na uimarishwaji wa uangalizi wa afya ya mimea.
‘’lengo kubwa katika mashirikiano hayo baina ya Wizara hizi mbili za Tanzania  na Afrika ya kusini ni kuhakikisha kwamba kilimo kinaimarika na kinachangia katika  usalama wa chakula na kuhakikisha kuwa kilimo kinaongeza  kipato cha wakulima” alisema Ndaba
Aidha Maeneo ambayo wamekubaliana kushirikiana ni maeneo la umwagiliaji,usalama wa chakula ,matumizi ya zana bora za kilimo,afya ya mimiea na chakula salama. Maeneo mengine ya ushirikiano ni uvuvi na afya ya wanyama ambayo mashirikiano hayo yataratibiwa baina ya  Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Wizaraya Kilimo ya Afrika ya Kusini. 

 

 

 

Muswada wa Umwagiliaji Wapitishwa

Muswada wa umwagiliaji(The National Irrigation Act, 2013)  uliowasilishwa na waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Eng. Christopher Chiza bungeni hivi karibuni hatimaye umepitishwa.
Akihitimisha katika hotuba yake waziri wa kilimo chakula na ushirika amesema muswada huo wa umwagiliaji utatatua matatizo na changamoto zinazoikumba sekta ya kilimo cha umwagiliaji na  utaleta mafanikio makubwa katika kilimo cha umwagiliaji Tanzania.
Aidha akichangia katika muswada huo, Mbunge wa Busega, Titus Kamani, alisema pamoja na Watanzania zaidi ya asilimia 80 kutegemea kilimo, taifa limekuwa likiishia kukosa chakula, na akasema sheria hiyo imecheleweshwa ili kujibu matakwa ya wakulima.
“Muswada huu umechelewa, lakini ni heri umeletwa na sheria ikipitishwa itakuwa ni neema kwa mikoa ambayo hukumbwa na ukame wa mara kwa mara. Kwa kuwa kilimo cha umwagiliaji, kitasaidia kuinua kilimo na kuongeza tija kwa wakulima,” alisema.
Hata hivyo, alitaka kujua fedha za uendeshaji wa Tume itakayosimamia umwagiliaji zitatoka wapi, kwa kuwa uhaba wa fedha umekuwa ukikwamisha mipango mizuri ya serikali.
Mbunge wa Mbarali, Modesti Kirufi akichangia muswada huo, alisisitiza kuwepo na mkakati wenye kuwakomboa si wakulima tu, bali hata wafugaji kwa kile alichodai kama sheria itapita, itawakomboa wakulima kutoka utegemezi wa mvua

 

 

WIAZARA YASAINI MKATABA WA KUINUA ZAO LA CHAI

Wizara wa Kilimo Chakula na Ushirika  na Kampuni ya  Univeler wametia saini ya makubaliano  ya kuanzisha ushirikiano wenye nia ya kufufua na kuendeleza tasnia ya chai hapa nchini.
Kwa mujibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika   Mhe. Eng . Cristopher Chiza ndani ya mkataba huo wakulima wadogo wa chai watanufaika kutokana na makubaliano hayo ambapo hekta 6,000 za mashamba ya chai  zinazomilikiwa na wakulima wadogo zitaboreshwa na kuongeza thamani  kwenye mauzo ya chai kwa zaidi ya thamani ya  Euro milioni 70  kwa mwaka.
Kupitia ushirikiano huu pia ajira zipatazo  5,000 zinatarajiwa kupatikana kwa wananchi wa Tanzania, aliongeza Mhe. Eng .  Chiza
“Kampuni ya Unilever itafanya kazi na wadau wote  wa tasnia ya chai hapa nchini ambao ni Serikali,Bodi ya Chai Tanzania na wakala waya Wakulima Wadogo wa Chai Tanzania kwa kushirikiana  wadau wengine katika Sekta za umma,  binafsi pamoja na wahisani”, alifahamisha Mhe. Eng .  Chiza
Mhe. Eng. Chiza alisema ubia huu unahusisha uwekezezaji katika maeneo ya mashamba yanayomilikiwa na kampuni ya Unilever na mnyororo wa thamani wa zao la chai unaoihusisha kampuni hiyo,ujenzi wa viwanda na miundo mbinu mipya katika maeneo ya uzalishaji,utafiti na maendeleo na program za kuwasaidia wakulima wadogo wa chai.
Ushirikiano huu utatekelezwa kupitia na kufadhiliwa na Mpango wa SAGCOT kama sehemu ya utekelezwaji wa Mpango wa Mageuzi katika Kilimo kupitia azma ya Kilimo Kwanza.
“Makubaliano haya yanaashiria dhamira ya Serikali ya Tanzania katika kutekeleza  azma ya kilimo Kwanza kwa lengo la kukifanya kilimo cha chai kuwa cha kibiashara kwa kuongeza fursa za kipato kwa wakulima wadogo na kusimamia vizuri matumizi ya rasilimali zetu za asili zilizopo” alifafanua Mhe.Chiza.  
Randama ya ushirikiano huu imetiwa saini mjini Dodoma na  Naibu Katibu Mkuu Eng. Mbogo Futakamba kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika na Afisa Mkuu Ugavi Kampuni ya Unilever Bwana Pier Luigi Sigismondi.

 

 

KADUMA KATIBU MKUU MPYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bib Sophia Kaduma kuwa Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.

Bib Kaduma anachukua nafasi  ilioachwa wazi na Bw. Mohamedi Muya ambaye amestaafu mwaka huu  kwa mujibu wa sheria.

 Aidha Mama Kaduma ni mzoefu katika wizara hii kwani amefanya kazi kwa muda mrefu kama Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa chakula na pia Naibu Katibu Mkuu.

Baadhi watumishi wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kwa nyakati tofauti wameupongeza uteuzi huo kutokana na uzoefu wake.

Mama Kaduma ana uzoefu wa miaka zaidi ya 20 ndani ya wizara hii akianzia kama afisa wa kawaida,  alishika nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Chakula na baadaye kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu.

Pamoja na uteuzi wa Mama Kaduma Rais Kikwete ameteua Maktibu wakuu wapya 11 na Naibu Makatibu 14.

 

 

Wakuu wa Wilaya Watakiwa Kutenga  Ardhi kwa Vijana

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Eng. Christopher Chiza amewaagiza Wakuu wa Wilaya kote  nchini kutenga ardhi ya kilimo kwa ajili ya vijana.
Mhe. Eng. Chiza ametoa agizo hilo kwenye uzinduzi wa sherehe za maonesho ya Nane Nane  katika viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Kufuatia agizo hilo  Wakuu wa Wilaya wa mikoa ya Dodoma na Singida kila moja alieleza jinsi gani ametenga ardhi ya kilimo kwa vijana katika wilaya yake.
Aidha, Mhe.Eng. Chiza, ametoa wito kwa vijana kujikita kwenye kilimo kwakuwa ni ajira nzuri inayoweza kuwainua kiuchumi na kuongeza kipato.
Akielezea mpango wa serikali kuwekeza kwenye kilimo kwa vijana,  amesema hivi sasa kuna vijana wengi waliomaliza  vyuo wamejikita kwenye kilimo na serikali imewasaidia kuwapatia ardhi kwa ajili ya shughuli za kilimo na  vijana hao wamekuwa ni mfano wa kuigwa na jamii nzima.
Pia aliwafahamisha vijana na wakulima kuwa kuna uhakika wa  soko la mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi  katika nchi ya Sudani Kusini kwa sasa.
“Mazao mengi yanayotoka Tanzania yanapendwa na watu wa Sudani Kusini” alisema Mhe.Chiza
Aidha  amewataka wakulima kuchangamkia fursa ya soko hili ikiwa ni pamoja na kuimarisha ufungashaji pamoja na uhifadhi wa mazao ili kuyaongezea thamani aliendelea kusema  Mhe. Chiza .
“ Changamoto kubwa katika kilimo ni upatikanaji wa masoko pamoja na usindiksaji wa mazao, wakulima wakiweza kuhifadhi  na kusindika mazao vizuri wataweza kuongeza ushindani na nchi za jirani ikiwemo Kenya ambayo inachukua mazao Tanzania na kuifunga upya hivyo kuonekana kama yanatoka kwao”,alisema Mhe. Chiza.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Eng. Mbogo Futakamba, ambaye alikuwa mkuu wa msafara wa ziara ya wakulima huko Sudani Kusini alielezea uhakika wa hali ya soko la mazao kuwa ni  mkubwa.
 Eng. Mbogo ameiomba serikali kufungua ubalozi wa Tanzania nchini humo ili wafanyabiashara wa kitanzania waweze kufanya biashara  kwa uhuru.

“Soko la bidhaa za kilimo nchini sudani ya kusini ni kubwa ili kutengeneza mazingira mazuri ya ki biashara ni vizuri serikali ya Tanzania ikaanzisha ubalozi wake humo, kwani wenzetu Kenya tayari wanaubalozi wao”,  alisema Eng.Mbogo

 

 

WIZARA  KUNUNUA MAZAO YA NAFAKA NCHINI

Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika imetangaza nia yake ya kutaka kununua mazao ya nafaka ili kumwekea mkulima wa hali ya chini soko la uhakika.
Miongoni mwa mazao yatakayonunuliwa kupitia Bodi  ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko  ni mpunga,maharagwe,karanga,choroko,ulezi,ufuta na mahindi,na yatanunuliwa kwa bei ya ushindani ya soko mwaka huu.
Hayo ni kwa mujibu wa Mchumi wa bodi hiyo Bw. Edwin Mkwenda  katika maonesho ya wakulima yaliyofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni Manispaa ya  Dodoma.
Bw. Mkwenda alisema tayari Serikali imeikabidhi bodi hiyo maghala yote yaliyokuwa ya Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC),ambayo hayakubinafsishwa zilizoko  kwenye kanda saba  ili kutunza mazao yatakayonunuliwa.
Kuundwa kwa bodi hiyo ni ukombozi kwa wakulima kwani watakuwa na uhakika wa kupata soko la mazao husika.

 

 

Umwagiliaji wa Matone kuongeza    Uzalishaji.

Serikali imepanga kuendeleza teknolojia ya Umwagiliaji wa Matone ili kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mazao kwa wakulima.
Akizungumza katika kilele cha maonesho ya sikukuu ya wakulima ya Nane Nane katika Viwanja vya Nzuguni mkoani Dodoma, Makamu wa Rais wa pili wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Iddy alisema kuwa umwagiliaji kwa njia ya matone utasaidia katika kukuza  uzalishaji wa mazao ya nafaka na bustani.
“Kutokana na teknolojia hii mpya ya umwagiliaji wa matone serikali imeweza kuvuna tani 16,510 za mazao kwa mwaka’’, alisema Balozi Seif.
Aliendelea kueleza kuwa teknolojia ya umwagiliaji ni lazima ipewe kipaumbele na kutekelezwa nchi nzima ili wakulima waweze kuzalisha mazao kwa wingi na kuuza ndani na nje ya nchi.

Aidha Balozi Seif aliwataka waandaaji na waendeshaji wa maonesho ya Nane Nane (TASO)  waweke utaratibu mzuri wa maonesho hayo ili wakulima waweze kuhamasika na kuhudhuria kwa wingi ili wapate mafunzo ya kilimo na ufugaji

 

 

ZANA ZA KISASA KUWAINUA WAKULIMA

Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika chini ya Idara ya Zana za Kilimo imeandaa mkakati wa kuboresha sekta ya kilimo ili wakulima waondokane na jembe la mkono na kutumia zana za kisasa ikiwa ni moja ya sababu zinazoweza kuleta tija kwenye sekta ya kilimo nchini.
Zana ambazo zimetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa na kutumia mafuta ya dizeli zinaweza kutumika katika mazingira mbalimbali ya kilimo nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya zana za kilimo ya Savoy Farm Ltd Bw. Omari  Issa akizungumza katika maonesho ya Nane Nane , viwanja vya Nzuguni alisema mashine aina ya ‘palleting’ zimetengenezwa kwa ajili ya kuwakomboa wajasiriamali wadogo wanaojishughulisha na kilimo ili wazitumie katika shughuli zao.
Alisema mashine hizo zinatumia muda mfupi katika kukoboa  mpunga na hivyo kurahisisha shughuli za mkulima.
‘’Tumetengeneza mashine za gharama nafuu ambazo zinawasaidia wakulima wa mpunga kukoboa nafaka kwa muda mfupi, hivyo aliwasihi wakulima  kuzitumia ili warahisishe shughuli zao za kilimo’’, alifafanua Bw. Omary.
Alifahamisha  kuwa mashine hizo zitasaidia kuongeza uzalishaji wa chakula katika maeneo mbalimbali nchini,na lengo la kutengeneza mashine hizo ni kuwawezesha  wakulima kuondoka kwenye matumizi ya  teknolojia ya zamani ya ukoboaji  kwa kutumia mikono na kujiunga kwenye teknolojia ya kisasa.
Kwa mujibu wa Bw. Omary mashine hizo zinatakiwa kwa wingi na  amewaomba wakulima kununua  zana bora za kilimo zinazotengenezwa nchini ili kupunguza gharama za kuagiza nje ya nchi.
Mmoja wa wakulima kutoka wilaya ya Manyoni  aliyehudhuria maonesho hayo  ,Bi. Salome Kazimoto alisema mashine za kukobolea mpunga zinasaidia kupunguza muda wa kukoboa kwa kutumia teknolojia ya zamani ambayo inachangia kurudisha nyuma  ufanisi wa kazi.
Bi. Kazimoto alikiri kuwa mashine hizo zinamrahisishia  kazi mkulima na kusema kuwa mpaka sasa idadi ya wakulima wanaotumia zana za kisasa ni wachache ikilinganishwa na idadi ya wanaotumia zana za zamani za kilimo.
Baadhi ya wakulima wanaoshiriki kwenye maonesho haya  ya kilimo wameitaka serikali kuelimisha wananchi ili watumie zana za kisasa katika shughuli zao.
‘’Endapo wakulima wataelimishwa ili watumie zana za kisasa za kilimo ili kujikwamua katika kilimo cha zamani kwa lengo la kuongeza uzalishaji’’aliongeza Bi. Kazimoto ambae ni mkulima.
Noel John, mkulima  kutoka  Morogoro alisema tangu  aanze kutumia mashine za kisasa katika shughuli mbalimbali za  kilimo katika zao la mpunga,amekuwa akifanya kazi hizo kwa muda mfupi na kwa ufanisi mkubwa.

 

 

Mbegu Zisizokizi Viwango ni Kikwazo katika Kumuinua mkulima

 

Utumiaji wa mbegu zisizokidhi viwango umechangia uzalishaji mdogo wa mazao kwa  wakulima wengi hapa nchini.
Akiongea na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika maonesho ya nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya nzuguni ,Dodoma Afisa masoko wa wa taasisi ya uzalishaji wa mbegu  ASA bib Jacquiline Itatiro amesema, matumizi ya mbegu feki yanatokana na    na uwezo  mdogo wa wakulima….. ukilinganisha na mahitaji, elimu ya matumizi za mbegu bora kwa wakulima pamoja na wasambazaji wa mbegu feki ambao sio waaminifu wanajitokeza kuuza mbegu zisizo na viwango katika kukidhi mahitaji ya mazao.
Aidha alisema usambazaji na uhamasishaji wa matumizi ya  mbegu bora kwa kushirikiana na sekta binafsi katika kuzalisha, kumechangia kumhamasisha mkulima kutumia mbegu hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zimeleta tija.
Hata hivyo alibainisha kwamba pamoja na kushirikiana na vituo vya utafiti kuhakikisha mbegu mpya zinazalishwa na zinamfikia mkulima bado miundombinu ya umwagiliaji maji mashambani imeendelea kuwa tatizo kwa wakulima hivyo kutegemea kilimo cha mvua za msimu.

 

Wizara Kushirikiana na Indonesia Kukuza Kilimo

Katibu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bi. Sophia Kaduma wa nne Kulia, akiwa  pamoja na Tume ya Ushirikiano wa Pamoja katika sekta ya kilimo.

 

Tume ya pamoja ya Ushirikiano katika sekta ya kilimo  ya Wizara ya Kilimo Chakula na ushirika imejadili maeneo ya kushirikina kwa awamu ya pili na serikali ya Indonesia  ili kuongeza tija na uzalishaji katika kilimo.

Akizungumza na tume kutoka pande zote mbili Tanzania na Indonesia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Mama Sophia Kaduma alisema majadiliano hayo yanalenga kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya kilimo pamoja na upatikanaji wa masoko.

Mama Kaduma alisema ushirikiano baina ya nchi hizo mbili utahusisha katika kujenga uwezo wa wakulima, masuala ya utafiti pamoja na upatikanaji wa masoko ya mazao.

Katika kujenga uwezo Mama kaduma alisema Tanzania na Indonesia itashirikiana katika mafunzo ya Muda mfupi na mrefu pamoja na kubadilishana wakufunzi ambao wataenda kufundisha vyuo mbalimbali vilivyopo katika nchi hizo.

Katika mafunzo ya muda mfupi serikali ya Indonesia itafadhili  masomo ya  Uchumi Kilimo na kilimo cha bustani hasa katika maeneo  ya utafiti, usindikaji na mbegu.

 
Alifafanua kukuwa Indosesi itafadhili mafunzo kwa wakulima 15 chini ya mpango wa Ushirikiano wa nchi za kusini   ambapo wakulima 12 watatoka Tanzania Bara na watatu watatoka Tanzania Visiwani.

Aliongeza kuwa masoma hayo yataanza tarehe 1-9/07/1213 na Tanzania itagharamia nauli za washiriki wa program hiyo pamoja na pesa za kujikimu.

Kwa upande wa mafunzo ya muda mrefu katika kujenga uwezo, serikali ya Indonesia itatoa ufadhili kwa watu watatu  ambao watasoma shahada ya uzamili na uzamifu na mmoja  ambaye atasoma masomo  yalio chini ya shahada ya kwanza.

Pia alisema nchi hizo mbili zitashirikana katika mambo ya utafiti wa mazao hasa katika mazao ya pamba, mpunga na viungo mbalimbali.

Alifafanua kuwa utafiti huo utahusisha mambo ya GMO, majaribioa mashambani, uzalishaji wa mbegu bora, magonjwa, usindikaji na uimarishaji wa vituo vya utafiti.

Mama Kaduma alisema pian nchi hizo zimekubalia kushirikiana katika katika masoko kwa kubadilishana taarifa za masoko na taratibu mbalimblia ili kuboresha biashara ya bidhaa za kilimo kati ya nchi zote mbili.

Alifafaunua kuwa licha ya kushirikiana katika masoko pia Serikali ya Indonesia itashiriki katika maonesho ya kimataifa ya wafanya biashara yafanyika Dar es Salaam (Sabasaba) pamoja na maonesho ya wakulima ya Nane Nane.

Ushirikianao baina ya nchi hizo mbili unalenga kuongeza tija katika kilimo, kuongeza upatikanaji wa masoko, kuongeza uzalishaji wa mazao pamoja na kukuza kipato cha mkulima.

 

 

Mifumo ya Asili ya Kilimo Kuendelezwa Kuinua Kilimo

Mazao yaliyostawi vizuri yakionyesha mojawapo ya aina ya kilimo Asili cha Mseto

Wadau wa kilimo, sera, mazingira, utawala, na mashirika ya kimataifa, wametoa wito wa kubaini mifumo asili ya Kilimo kwa kutambua mchango katika uhakika wa chakula na kipato.

Wito huo ulitolewa katika warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliyojumuisha wadau hao ili kutathmini mchango wa mifumo asili ya kilimo na changamoto zilizopo ili kuiboresha na kiendeleza.

Ilibainika kuwa Tanzania ina mifumo mingi ya asili ya kilimo na mifugo ambayo imedumu kwa taribani zaidi ya miaka 100 hadi 700.

Katika kipindi hicho, mifumo mingi imekumbana na mabadiliko ya hali ya hewa lakini imekabili na kudumu, hii inaonyesha kuwa kuna vitu vingi vya kujifunza katika mifumo hiyo.

Aidha, wadau wamependekeza mifumo ya asili ya kilimo na ufugaji kuingizwa katika sera kati ya zilizopo ili ipate nguvu ya kusimamiwa na kuendelezwa hasa ikizingatiwa umuhimu wake katika kuimarisha usalama wa chakula na kipato kwa kaya na taifa kwa ujumla.
 
Pia wametaka mashirika ya kimataifa yaendelee kuchangia kwa rasilimali uendelezaji wa mifumo asili endelevu kwani manufaa yake ya mazingira ni ya ulimwengu.

Afisa Mkuu wa Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Firmat Banzi alisema kuwa mifumo asili ya kilimo ina haja ya kuendelezwa ili kuboresha na kuimarisha maarifa asili kuwezesha ushiriki wa wakulima katika utunzaji wa mifumo hiyo.

Alifafanua kuwa uendelezaji wa mifumo hiyo utawapa fursa wakulima kuweza kushiriki kikamilifu katika kilimo wakiwa na uhakika wa kupata mazao mengi kuweza kujitosheleza kwa chakula na kujiongezea kipato pamoja na kuboresha hifadhi ya mazingira hasa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Washiriki kwa pamoja wamepitisha azimio linalotambua mchango wa mifumo ya asili ya kilimo na ufugaji na wametoa wito wa kubaini mifumo asili iliyopo nchini, kutathmini mchango wake na changamoto kwa lengo la kuiboresha na kuiendeleza.

 

 

Wakulima na Wafanyabiashara Kuhudhuria Maonesho ya Kilimo Sudani ya Kusini

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Eng Christopher Chiza katika picha ya pamoja na msafara wa watu 14 waliokwenda ziara ya mafunzo ya kilimo Sudani ya Kusini, Kulia ni Katibu Mkuu Bibi Sophia Kaduma.

 

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika imepeleka wakulima na wafanya biashara wa mazao ya kilimo wapatao 14 katika ziara ya mafunzo katika nchi ya Sudani Kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza alisema hatua hiyo imekuja baada ya kupata mualiko kutoka kwa Waziri wa Kilimo wa nchini Sudan Kusini walipokuwa katika mkutano wa Jukwaa la Mapinduzi ya Kijani (Agra) uliofanyika mjini Arusha.

 “Tumewateua ninyi muwe mabalozi wetu huko Sudan Kusini ili mtakaporejea muweze kuwafikishia wakulima wetu yale mtakayojifunza huko, pia muainishe mazao ambayo yana masoko kwa wingi nchini Sudan.”alisema waziri.

Waziri alisema kuwa mazao mengi ya Tanzania yamekuwa yakipatikana nchini Sudan kama vitunguu, na mchele  kwa bei ya juu lakini mkulima wa Tanzania  anakuwa hafaidiki hivyo kuwataka kuainisha fursa za masoko ili kuongeza kipato.

Waziri aliwahimiza wakulima na wafanyabiashara hao kuainisha fursa mbalimbali ambazo wakulima wa Tanzania wanaweza kunufaika nazo.

Wakulima kwa upande wao wameishukuru Serikali kwa kuwapatia fursa hiyo muhimu ambayo itawawezesha kujifunza na kuahidi kuwa mabalozi wazuri wa wakulima nchini na kuwa chachu ya mabadiliko pindi watakaporejea.

Wakulima na wafanyabiashara wametakiwa kuangalia uwezekano wa kuongeza tija katika mazao kwa kusindika mazao na kuweka nembo ya Tanzania. Aidha, wakulima wametakiwa kutokuuza mazao mashambani kiholela bali wavune na kuyaongezea thamani.

Naye mkuu wa msafara huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Eng.  Mbogo Futakamba alisema wakulima na wafanyabiashara hao watapata nafasi ya  kuangalia na kujifunza  vikwazo vya kibiashara vilivyopo nchini Sudan ya Kusini ili kuweza kuvifanyia kazi watakaporejea nchini ili kurahisisha ufanyaji biashara nchini humo.

“Ziara hii ya mafunzo itawapa fursa wafanyabiashara na wakulima kujifunza uendeshaji biashara na pia watahudhuria maonesho ya wakulima” aliongeza  Futakamba.

Msafara huu pia utajumuisha wakuu wa wilaya ya Bahi Betty Mkwasa na wilaya ya Kakonko Ndugu Peter Toima  Kiroya na  utaongozwa na Naibu katibu Mkuu toka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Eng. Mbogo Futakamba, ziara hiyo ni  ya siku tano.

 

 

AMAGRO Yakabidhiwa Vifaa  vya Kupambana na Nzi wa Embe

Mtaalamu kutoka kitengo cha uthibiti  Visumbufu wa Mimea Kibiolojia Nsami Elibariki akitoa maelezo ya matumizi sahihi ya moja ya vifaa vilivyotolewa na Kituo cha Kimataifa cha Uthibiti Wadudu Waharibifu wa Mazao.


Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika imekabidhi vifaa vya  kupambana na Nzi wa embe kwa Chama cha Wakulima wa Embe (AMAGRO) ili kuboresha kilimo cha embe hapa nchini, hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Mikocheni kilichopo Jijini Dar es Salaamu.
Awali Mratibu wa  Mradi wa Udhibiti Nzi wa  waharibifu wa matunda kutoka kitengo cha Afya ya Mimea cha Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Janet Muganyizi alifahamisha kuwa vifaa hivyo vimetoka  Kituo cha Kimatasifa cha kuthibiti Wadudu waharibifu  (ICIPE) chenye makao makuu yake Nairobi nchini Kenya.
Kwa mujibu wa Muganyizi kituo hicho pia kilitoa mafunzo kwa wakulima  huko Kibaha mkoani Pwani  ikiwa ni sehemu ya msaada wa kituo hicho kuboresha kilimo cha embe hapa nchini  miongoni mwa wakulima wa Tanzania.
“Jumla ya wakulima 150 toka ktika mikoa 15 watanufaika na msaada huo muhimu wa kukabiliana na Nzi wa Embe mingoni mwa wakulima wa zao hili” alifahamisha Muganyizi katika hotuba yake ya kumkaribisha mgeni rasmi.

Aliitaja baadhi ya mikoa hiyo kuwa ni   Mbeya, Dar es Salaamu, Pwani, Morogoro, Tanga, Tabora, Dodoma, Mwanza , Iringa, Kilimanjaro, Songea,  Arusha na Lindi.
Vifaa vilivyokabidhiwa katika hafla hiyo kuwa ni lita 20 za kivutia madume, lita 40 za chambo  na mitego 3,000, vikiwa na thamani ya Dola za Kimarekani 6,071 ambayo ni sawa na zaidi ya 9,700,000 zikiwa gharama za ununuzi, alifahamisha Muganyizi.
Naye mgeni rasmi katika hafla hiyo ya makabidhiano ya vifaa hivyo Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao toka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bwana Beatus Malema aliwataka wakulima wa embe walionufaika na msaada wa vifaa hivi kuwa  viwe ni mchangamoto katika kuboresha uzalishaji wa embe zenye ubora ili kuweza kushinda na  kupata nafasi  katika soko la Afrika Mashariki na Dunia.
“ Huu ndio mwanzo kwa ndugu zangu wakulima kuboresha  zao la embe ili tuweze kupiga hatua na kupata soko la uhakika kwa maufaa yetu wenyewe”  aliongeza  Malema
Malema aliwataka wakulima kufuata misingi bora ya uazalishaji wa zao hili ikiwemo usafi katika shamba, kutumia wadudu rafdiki wa mkulima wanaoshambulia Nzi hawa na kwa kutumia mitego ya kunasa Nzi wa embe.
Pia  aliwataka wakulima kuyatumia mafunzo wanayopata toka kwa watalaamu wa kilimo ili kuboresha zao hili la embe kwani vinginevyo wataishia kulima kilimo kisicho na tija.
“ Tukiamua kufanya kweli kuboresha zao la embe tunaweza kubadili maisha yetu na kutoka hapa tulpo katika maisha yetu”  Malema aliwasisitiza wakulima hao.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wa Embe hapa nchini  ndugu Burton Nsape aliishukuru sana serikali kwa msaada huu muhimu kwa wakulima wa embe hapa nchini, ambao utawasaidia sana kuboresha zao hili na pia utakuwa mwanzo wa kupambana na mdudu Nzi.
“Msaada huu mliotupa utakuwa changamoto kubwa kwao kuboresha zao hili kwa manifaa yao na Taifa kwa ujumla” alisisitiza Nsape wakati akitoa shukrani zake kwa serikali kwa niaba ya wanachama wenzake.
Pia Nsape aliitika serikali issiishie hapa bali iweze kuwafikia wakulima wengine wadogo ili kuboresha kilimo cha zao la embe miongoni mwa wakulima hapa nchini.
Naye mtalaamu wa kilimo toka kitengo cha Uthibiti Visumbufu wa Mimea Kibaolojia  katika kituo cha Kibaha mkoani Pwani Nsami Elibariki aliwataka  wakulima kufuata taratibu za matumizi sahihi  ya vifaa hivi ili kuboresha zao la kilimo cha embe.
Chama cha Wakulima wa zao la Embe kilianza mwaka 2001 kwa kuwa wanachama toka mikoa 15 ya hapa nchini kikwa na lengo kuu la kuboresha kilimo cha embe kwa kuwatanisha wakulima wa zao hili kupambana na changamoto ya kilimo cha zao hili.

 

 

 
 

Chiza Ainisha Fursa za Kilimo

Waziri wa Kilimo Chaklula na Ushirika Mhe. Eng Christopher Chiza akiongoza mkutano wa wataalamu kutoka Uturuki na maafisa wa wizara hiyo, kulia ni waziri wa Chakula Kilimo na Mifugo wa Uturuki Mhe. Mehdi Eker.

 

 

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Eng. Christopher Kajoro Chiza ameainisha fursa za kilimo ambazo inaweza kushirikiana na serikali ya Uturuki katika kuinua kilimo hapa nchini.

Eng. Chiza aliyasema hayo wakati akizungumza na ujumbe maalumu kutoka  Uturuki ukiongozwa na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Mehdi Eker, ambao ulifika Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kubadilishana mawazo katika kushirikiana uboreshaji wa kilimo.

Moja ya fursa alizobainisha ni pamoja na uwekezaji wa sekta binafsi katika kilimo, sekta ambayo bado haijafanya vya kutosha katika kuinua kilimo.

“Tanzania ina eneo kubwa la kuwekeza katika kilimo lakini bado sekta binafsi haijachukua nafasi yake katika kuinua kilimo” aliongeza Eng. Chiza

Miundo mbinu katika kilimo cha umwagiliaji maji ni sehemu moja ambayo serikali ya Tanzania inaweza kushirikiana na Uturuki na watu wake katika kuboresha kilimo hapa nchini kwa kujenga miundo mbinu bora katika kilimo.

“Bado nchi yetu ina miundo mbinu hafifu  ya teknolojia ya matumizi ya maji katika kuinua kilimo hapa nchini” alifahamisha Eng. Chiza.

Mheshimiwa Eng. Chiza aliitaka pia serikali ya Uturuki kushirikiana na Tanzania katika kuanzisha mpango kabambe wa kuwashirikisha vijana wa Tanzania katika kuinua kilimo hapa nchini.

“ Vijana wetu wanahitaji kupewa moyo ili washiriki kikamilifu katika shughuli za kilimo ili kweli tuweze kufanikiwa katika kilimo chetu kwani vijana ndio nguvu kazi,” aliainisha Mhe. Chiza.

Eneo lingine ambalo Mhe. Eng. Chiza aliuambia ujumbe wa Uturuki kuweza kushirikiana na Tanzania ni kilimo cha maua.

Aliongeza kuwa mfumo wa usafirishaji wa bidhaa za maua hadi katika soko lake bado ni tatizo nchini kwetu, hinyo aliomba Uturuki kushirikiana na Tanzania katika eneo hili ili kuinua kilimo hiki.

Mbali ya fursa hizo pia  Mhe. Eng. Chiza pia aliwafahamisha wajumbe kuwa matumizi ya zana bora za kilimo bado ni kiwango cha chini sana, kwani ni wakulima asilimia 10 tu wanatumia zana bora katika kilimo zikiwemo tractor.

Awali aliwafahamisha  wajumbe hao kuwa   Tanzania ina eneo zaidi ya   milinoni 44  linalofaa kwa kilimo lakini ni asilimia 25 tu linatumika.

Serikali ya Uturuki kupitia ujumbe huo  imeonyesha nia ya kushirikiana Tanzania katika sekta ya umwagiliaji, uzalishaji wa mbegu na kuwekeza katika uzalishaji wa mbolea.

Maeneo mengine ambayo serikali ya Uturuki  imesema kuwa iko tayari kufanya kazi kwa kushirikiana na  serikali ya Tanzania kuwa ni eneo la afya ya mimea, kilimo cha maua na mifugo.

Maamuzi yaliyofikiwa katika mkutano huo ni kuunda kamati maalumu kwa kushirikisha watalaamu wa Tanzania na Uturuki ili kuchambua na kuona maeneo ya kushirikiana katika kuinua kilimo.

 

Wizara Kufufua Mifumo Asili ya Kilimo

Mfumo wa Kilimo cha asili aina ya Kiamba unaotumiwa na kabila la Wachaga.

 

Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika imeanzisha Mradi wa kufufua Mifumo muhimu ya asili ya kilimo Duniani (Global Importance Agricutural Heritage System- GIAHS) ili kuendeleza Kilimo cha asili (Oranic Farming) na kumpunguzia mkulima gharama za uzalishaji.

Mradi huo unatekelezwa na Shirika la chakula Duniani (FAO) ambao unalenga kutambua mifumo ya asili na endelevu ya kilimo na ufugaji ili kumsaidia mkulima.

Afisa Mkuu wa Kilimo kutoka Idara ya Matumizi Bora ya Ardhi Bw.  Firmat Banzi
alisema mradi unagharimu zaidi ya dola laki mbili ambazo zimetolewa na Serikali ya Ujerumani.

Alisema kuwa katika Afrika Mashariki nchi ya Tanzania na Kenya ilichaguliwa kufufua mifumo hiyo kwa kuwa na sehemu muhimu za kilimo zanazotumia mifumo hiyo.

Aliongeza kuwa baada ya kuchanguliwa nchi ya Tanzani ilipendekeza mifumo mitatu ya kilimo asili ambayo ni Kihamba ambao hutumiwa na wachaga, Ndiva wa Wapare na Ngoro ambao hutumiwa na kabila la wamatengo.

Alifafanua kuwa mifumo hiyo mitatu ilifanyiwa utafiti na baadaye mfumo wa kichanga ulichaguliwa na kuanza kutumika. 

Aidha, alisema kijiji cha Chimbe juu kilichopo wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro ndio kilichonufaika na mradi huo na sasa unafikia hatua ya mwisho katika utekelezaji wake.

Hatua hiyo imekuja baada ya tafiti mbalimbali kuonesha kushuka kwa bei ya zao la kahawa na kusema kuwa kilimo asili huongeza bei za mazao kwa kuwa mazao yanayolimwa hayatumii kemikali na badala yake hutumia mbolea ya asili kama vile samadi, aliongeza Bw. Banzi.

Mradi huo utasaidia kuboresha zao la kahawa kwa kutumia mbinu husishi za  kukabiliana na wadudu waharibifu wa mazao.

Alifafanua kuwa  mradi unajumuisha utayarishaji wa vitalu vya miche, ukarabati wa mifumo asili ya umwagiliaji na utayarishaji wa mbolea za asili kama vile samadi.

Ili kuhakikisha mradi huu unaendelea Bw. Banzi alisema wameshirikisha wadau mbalimbali ambao watasaidia kuangalia kwa karibu maendeleo ya mradi, alitaja wadau hao kuwa ni Chama cha Ushirika KNCU cha Kilimanjaro pamoja na halmashauri ya wilaya.

Mifumo ya asili ya kilimo ilianza kupendekezwa dunia toka mwaka 2002 na baadhi ya nchi zimeanza kutumia mifumo hii, baadhi ya nchi hizo ni Japani, Philipino, China na Ujerumani.

 

 

 
 

Mafunzo ya Nanenae Yawafurahisha Wakulima

Wakulima wamefurahia mafunzo mbalimbali ya kuendesha  kilimo  yaliyokuwa yanatolewa katika maonyesho ya wakulima Nane Nane yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Nzuguni mkoani Dodoma.
Wakulima hao, waliongeza kuwa licha ya kujifunza mambo mbalimbali pia wameweza kupata mbembejeo za Kilimo kwa bei nafuu na kwa urahisi.
Alisema wakulima wameweza kujifunza mambo mbalimbali katika mashamba darasa yaliyoandaliwa na maofisa Kilimo kama mfano kwa wakulima waliokuja katika maonyesho hayo.

“Nimefurahia sana maonyesho hayo kwani yameniwezesha kupata pembejeo kama vile mtambo wa kupukuchi mahindi (global cycle solution) ambao unazwa kwa bei nafuu”, alisema Bwana Alex Sori mkulima wa mahindi kutoka Hombolo.
“Kwa kweli maonyesho haya yameniwezesha kujivunza vitu mbalimbali na jisi ya kukufanya Kilimo changu kuwa cha kisasa zaidi, nimejifunza aina mbalimbali za mbegu na jisi ya kuzipanda ili kuniwezesha kuweza kuvuna mzao mengi”, alisema Bwana Edwini Makaya mkulima kutoka wilayani Chamwino.
Aliongeza kuwa wameweza kujifunza aina mbalimbali za mbegu na jisi ya kupnda katika utaalaamu ambao utawawezesha kuvuna mazao mengi yatakoayoweza kuwaongezea kipata chao.

Bwana Sori aliwashauri wakulima kujenga tabia ya kutembelea maonyesho hayo kwani watawawezesha  kupata mbegu bora na kwa bei nafuu.
Pia alisema kupitia maonyesho hayo ameweza kujifunza teknolojia mbalmbli ambazo ni za kisasa kama vile Kilimo cha umwagiliaji na jinsi ya kutumia zana bora za Kilimo zikiwemo matrekta.

“Hakika maonyesho haya yamenipatia elimu ya namna ya kutumia zana mbalimbali za Kilimo ambazo nimekuwa sijawahi hata kiziona na nilizokuwa nazisikia, leo hii niomeweza kuziona kwa macho yangu na kupatiwa mafunzo ya jinsi ya kuzitumia”, alisema Bibi Magreti Haule, mkulima kutoka Wilayani Kongwa.
Katika maonyesho hayo wakulima pia waliweza kujifunza jinsi ya kudhibiti waduu waharibifu katika mazao mbalimbali kwa kutumia madawa ili kupunguza uharibifu wa mazao.

 

 

Wakulima waaswa juu ya Sensa ya maendeleo ya Kilimo

Wakulima na wadau wa Kilimo wameaswa kutopuuza zoezi la Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika tarehe 26 mwez huu.
Wito huo ulitolewa na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal katika kilele cha sherehe sikukuu ya wakulima Nane nane iliyofanyika katika viwanja vya Zuguni, mjini Dodoma.
Aidha Dkt Bilal aliwataka wakulima pamoja na wadau wote wa Kilimo kutoa ushirikiano kwa wahudumu wa Sensa ili kufanikisha zoezi hilo muhimu.
“Sensa  ni muhimu katika maendeleo ya nchi na pamoja na watu wake kwani inawezesha Serikali na wadau wake kupanga mikakati sahihi ya maendeleo kwa manufaa ya wote”, Alifafanua Dkt Bilal.
Hata hivyo Dkt Bilal alifafanua kuwa  katika  Sekta ya Kilimo hutoa fursa ya kutambua idadi ya  wakulima na wadau wote wanaotoa huduma katika sekta ya Kilimo ili kupanga mipango katika kuboresha sekta hiyo.
Katika hotuba aliyoitoa Dokta Bilal katika maadhimisho hayo aliwataka wakulima na wadau wengine wa Kilimo kutumia nafasi hiyo muhimu  walionao hasa wakiwa ni sehemu kubwa ya Watanzania  kutoa maoni katika kufanikisha zoezi la ukusanyaji maoni kwa ajili ya Katiba mpya.

 

 

Msukumo wa Pamoja ni Muhimu Katika Kuongeza Uzalishaji wa Mpunga

Wakulima wametakiwa kuweka msukumo wa pamoja ili kuhakikisha kwamba zao la mpunga linaendelezwa kwa kiwango kikubwa ili kuinua kiasi cha uzalishaji na kuongeza usalama wa chakula na kipato.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. E.ng. Christopher Kajoro Chiza alipokuwa akiwahutubia mamia ya wakulima waliohudhuria maadhimisho ya maaonyesho ya zao la mpunga yaliyofanyika katika uwanja wa Mnazi mmoja jijini Dar es salaama
Aidha msukumo huo utawasaidia wakulima kuendeleza uchumi na kuwakwamua wananchi walioko katika ukanda wa mashariki mwa Afrika kutoka kwenye umaskini hususan kwa wakulima wadogo ambao wanahitaji kupata teknolojia mbalimbali zinazoweza kuwasaidia katika kuongeza uzalishaji na tija.
‘Hapa kwetu tunatambua umuhimu wa zao la mpunga. Zao hili ni la pili kwa uzalishaji katika mazao ya nafaka baada ya zao la mahindi na hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Mwanza, Mbeya, Rukwa, Morogoro, Arusha, Manyara, Iringa, Mara, Tanga na Kigoma. Aidha uzalishaji wa mpunga unaongezeka mwaka hadi mwaka na takwimu zinaonyesha kwamba eneo la uzalishaji liliongezeka kutoka hekta 490,000 mwaka 1998 mpaka hekta 854,000 mwaka 2011’.
Waziri alisema kuwa  mwaka 2010/2011 uzalishaji wa Mpunga ulifikia wastani wa tani 2,213,020.  Hii inaonyesha uzalishaji wa mpunga unaongezeka kwa kasi kubwa kutokana na kuongezeka kwa ruzuku kwenye mbegu, mbolea pamoja na kupanuliwa kwa eneo la umwagiliaji ambalo kwa sasa limefikia hekta 381,000 ambalo kwa sehemu kubwa linalimwa zao la mpunga.
Inakadiriwa kuwa ongezeko la matumizi ya zao la mpunga kama chakula duniani ni zaidi ya asilimia 6 kwa mwaka. Kwa Tanzania mahitaji yetu ya mchele kwa mwaka 2009/2010 yalikuwa tani 788,570 ikilinganishwa na uzalishaji wa tani 1,699,830. Mwaka 2010/2011 mahitaji yaliongezeka na kufikia  tani 816,648 ikilinganishwa na uzalishaji wa tani 1,461,648 alisema Mh. Chiza.

 

Kuongezeka kwa Bei ya Bidhaa za Nafaka ni Furusa kwa Wakulima

Kupanda kwa bei ya bidhaa za chakula kama mchele na mahindi mijini kwa kiasi kikubwa kumechangiwa  na kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa hizo katika nchi jirani.
Hayo yamesemwa na waziri wa Kilimo chakula na ushirika Mh.Christopher Chiza alipokuwa anaongea na waandishi wa habari katika uwanja wa Mnazi mmoja hivi karibuni
Chakula kutoka Tanzania kimekuwa kikisafirishwa katika nchi za Sudani, Somalia na baadhi nchi jirani hivyo kusababisha ongezeko la mahitaji ya chakula na kufanya bei yake kuwa juu.
Aidha,  bei ya mchele mijini hususan katika jiji la Dar es Salaam imefikia shilingi 2,300 kwa kilo. Pamoja na jitihada za kuingiza mchele kutoka nje, bei yake na hata mahindi haijashuka. Hii ni ishara ya mahitaji makubwa ya nafaka (hasa mchele na mahindi) katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na Pembe ya Afrika.
Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji kutoka katika nchi za jirani, wakulima na wadau wa kilimo nchini Tanzania wametakiwa kutumia fursa hiyo kuongeza uzalishaji kwa kuwa kuna uhakika wa soko la mazao hayo.

 

 

Mkakati wa Kupambana na Changamoto za Zao la Mpunga

Wizara ya Kilimo chakula na Ushirika na wadau wake imeanzisha  mkakati wa kuendeleza zao la mpunga (National Rice Development Strategy – NRDS) ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo mara dufu ifikapo 2018.
Waziri wa kilimo chakula na ushirika Mh. Eng. Christopher Chiza ametaja upatikanaji mdogo wa mbegu bora kama mojawapo ya changamoto inayokumba zao la mpunga, wakati akiwahutubia wakulima na wadau wa zao hilo ambao walihudhuria maonyesho ya zao la mpunga yaliofanuyika katika uwanja wa Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam yaliyoanza tarehe 18-22 Juni 2012.
Changamoto nyingine ni upatikanaji mdogo wa teknolojia bora za uhifadhi na ufungashaji  (grading and packaging) pamoja na kutokuwepo kwa miundombinu ya umwagiliaji ya kutosha kuongeza uzalishaji wa mpunga alisema Mh. Chiza.
Aidha,  ukosefu wa  masoko ya uhakika  na teknolojia duni za usindikaji zimekuwa zikirudisha nyuma juhudi za wakulima kuuza mazao yao yakiwa ghafi badala ya kuuza kama bidhaa.
Katika mkakati huo maeneo ya kipaumbele ni kuboresha uzalishaji wa mbegu bora, umwagiliaji maji, matumizi ya zana za kisasa, uongezaji thamani kwa zao la mpunga, huduma za ugani na utafiti na masuala ya masoko na mikopo katika kuendeleza zao la mpunga.
Ukosefu wa mikopo kwa wakulima, imekuwa inachangiwa kwa kiasi kikubwa na masharti magumu yanayotolewa na taasisi za kifedha, hivyo wakulima kukosa mitaji ya kuwekeza katika  kilimo alisema Mh Chiza.
Matumizi madogo ya teknolojia rahisi na kasi ndogo ya kusambaa kwa teknolojia miongoni mwa wadau, masuala mtambuka kama maambukizi kwa virus vya Ukimwi na Malaria, pamoja na Ushiriki mdogo wa sekta binafsi katika kilimo ni changamoto  ambazo zinahitaji jitihada maalum katika kuimarisha sekta ya kilimo hapa nchini,  alihitimisha Mhemiwa Waziri.

 

Wizara Yapata Mawaziri Wapya

Mheshimiwa Eng. Christopher Kajoro Chiza Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika (kushoto), Naibu Waziri wake Mheshimiwa Adam Malima (katikati) na Makatibu Wakuu wawili wa Wizara hiyo wakati wa mapokezi ya mawaziri hao baada  yakuwasili makao makuu ya wizara wakitokea  viwanja vya Ikulu walipokuwa wakiapishwa  hivi karibuni

 

Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika imepata Mawaziri wapya baada ya kuhamishwa wizara aliyekuwa waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mheshimiwa Prof Jumanne Maghembe na kuwekwa  Mhandisi Christopher Chiza ambaye hapo mwanzo alikuwa ni Naibu waziri wa wizara hii.

 Mheshimiwa Adam Malima ambaye hapo mwanzo alikuwa Naibu waziri wa wizara ya Nishati na madini kwa sasa ndiye Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.

Mabadiliko hayo yamekuja hivi karibuni baada ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete kuvunja Baraza la Mawaziri siku ya tarehe 4 Mei mwaka huu Ikulu jijini Dar es Salaam na kuunda baraza jipya.

Baada ya kufika wizarani kutokea Ikulu walipokuwa wanaapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Mawaziri hao waliongea na wakurukungezi na wakuu wa Idara na Vitengo ambapo Waziri mpya wa Wizara ya kilimo Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza alisisitiza kuimarishwa ushirikiano baina ya wafanyakazi ili kufikia malengo walijiwekea

 “Ushirikiano ni chombo kitakacho tupeleka sehemu tunayotaka kwenda ,hivyo ni muhimu kuimarishwa ushirikiano baina yetu ili kuziimarisha huduma zetu. Kila mtumishi asimamie majukumu yake kikamilifu na kwa kufanya hivyo ndipo tutakapo weza kufikia malengo yetu” alifafanua Mhandisi Christopher Chiza.

Kwa upande wake Naibu  Waziri  Mheshimiwa Adam Malima amewataka watumishi wote pamoja nakutekeleza majukumu kiufasaha kuwepo na uwazi katika utendaji wa kazi kama njia rahisi ya kutatua matatizo.

“Uwazi ni jambo zuri sana katika utendaji wa kazi, kwani utatuwezesha kutatua matatizo mbalimbali yatakayokuwa yanatukabili alisema Mheshimiwa Adam Malima.

 

 

 

Naibu Waziri  Aipongeza  ASA

Waziri wa kilimo Chakula na Ushirika   Christopher Kajolo Chiza (Mb) amezipongeza juhudi zinazofanywa na  ASA katika juhudi za serikali za kuongeza uhakika wa  upatikanaji wa mbegu bora hapa nchini,, kwa lengo la kupunguza utegemezi kutoka nchi zingine. Aliagiza kuza kuwa kuwepo na juhudi za makusudi za kuwashirikisha wakulima wadogo kuzalisha mbegu za kuazimiwa (QDS)

Naibu Waziri vile vile aliwagiza Wahandisi wa Umwagiliaji kufanya uchunguzi (survey) katika mashamba ya Msimba kuhusiana na  ujenzi wa miundombinu ikiwa ni pamoja utokaji wa maji (drainage) kwa lengo la kumwagilia mashamba ya mbegu ili kupunguza utegemezi wa mvua.

Naibu Waziri alimwagiza mchimbaji wa visima kufanya majaribio ya matumizi ya Pampu kutoa maji visimani (pump test) ili kazi zingine zinazohusiana na umwagiliaji zianze mara moja.

Mafunzo kuhusu Mtambo wa Kupokelea Mawasiliano

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Bibi Lilian Mapfa jana alifungua rasmi mafunzo ya uelewa kuhusu mtambo wa kupokelea taarifa za hali ya hewa  wa Wizara.

Mafunzo hayo yanaendeshwa na Kitengo cha Mazingira kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA)
yana lengo la kuongeza uelewa kuhusu masuala ya taarifa za hali ya hewa ambapo Wizara itakuwa na uwezo wa kutoa taarifa sahihi za kiwango cha mvua kwa wakulima wa Tanzania.

Bibi Lilian alisema  lengo la mafunzo hayo yanayofanyika katika Chuo cha Utalii, Tandika ni kuongeza uwezo wa kufuatilia, kujiweka tayari ili kukabiliana na mabadiliko ya kimazingira ikiwemo hifadhi endelevu ya mazingira inayochangia kupunguza umaskini.

Bibi Mapfa aliongeza kuwa mtambo huu utasaidia kufanikisha shughuli za kilimo, utafiti katika kilimo hasa mbegu.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mazingira cha Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Bibi Shekwanande Natai alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia Wataalam wa Wizara kujua namna ya kutumia mtambo huo na faida zake.

Wahandisi Umwagiliaji,  Wasaidie  Kuibua Miradi ya Umwagiliaji

Naibu Waziri wa Kilimo chakula na Ushirika Mhe. Christopher Kajolo Chiza amewagiza Wahandisi wa Umwagiliaji,  Kuwawezeshe wakulima kuibua miradi ya umwagiliaji.

Hayo aliyasema wakati akifungua mafunzo ya wiki mbili ya Wahandisi wa Umwagiliaji wa Umwagiliaji wa Kanda, Sekretariati za Mikoa na Halmashauri za wilaya, yaliyofanyika mjini Morogoro hivi karibuni

Mhe. Chiza aliagiza kuwa fedha zinazotolewa kwa ajili ya  miradi ya umwagiliaji lazima zitumike kama zilivyokusudiwa.

Alisisitiza kuwa  wakulima wajulishwe  kiasi cha fedha kinachotumika katika miradi ya umwagiliaji, maana ya mifuko (Vyanzo vya  fedha)  ikiwa ni pamoja na umoja wao unaowawezesha kutekeleza vizuri miradi ya umwagiliaji.

Aidha Mhe. Chiza alisema kuwa serikali inalenga kuwa ifikapo mwaka 2015 asilimia 25 ya chakula chote kinachozalishwa nchini kitokane na  kilimo cha Umwagiliaji, kwa kuongeza maeneo ya kilimo hicho kufikia hekta 1,000,000, na vile vile kulima kisasa katika maeneo yalioyopo

 

 

 

Kamati ya Bunge Yatoa ushauri Kwa Wizara

Kamati ya Bunge iliyotembelea Wakala wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) hivi karibuni wameishauri Serikali kuongeza juhudi katika kusambaza chakula cha msaada kwa waathirika wa njaa katika Wilaya na Halmashauri zilizokumbwa na tatizo hilo.
Wakiongea kwa nyakati tofauti Wajumbe wa Kamati hiyo wamesema kuwa inachukua muda mrefu kwa chakula cha msaada kuwafikia walengwa kwa sababu ya kuwepo kwa kamati nyingi za ugawaji wa chakula hicho hivyo kuzidi kuwapa hali ngumu walengwa.
Aidha Wajumbe wa Kamati hiyo wamesistizia Idara ya Usalama wa Chakula kutoa ushirikiano mkubwa  kwa  Halmashauri wakati wanapofanya tathimni ili kupata Idadi kamili ya waathirika wa njaa na kuepuka taarifa zisizo sahihi.
Naibu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Kilimo Chakaula na Ushirika  Bibi Sophia Kaduma aliieleza Kamati ya Bunge ya Kilimo Maji na Mifugo kuwa  changamoto kubwa kwa Wakala wa Hifadhi ya Chakula ni upatikanaji wa magunia ya kuhifadhia nafaka na idadi ndogo ya maghala.
Alibainisha kuwa kiwanda kinachozalisha magunia ya katani hapa nchini hakina uwezo wa kutosha wa kuzalisha, hivyo kushindwa kusambaza magunia katika taasisi za Wizara ya Kilimo hasa ikizingatiwa kuwa Wizara ina uhitaji mkubwa wa magunia ya kuhifadhia kahawa, pamba na mazao mengineyo katika tasisi zake.
Kuhusu uhaba wa chakula Bibi Sophia Kaduma  amesema kuwa tathimini hufanywa  mapema pindi taarifa zinapopatikana kutoka katika vyanzo  husika.

Wilaya ambazo zimepata upungufu wa chakula zimeshafanyiwa kazi na Wilaya nyingine zilizojitokeza na zinazoendelea kujitokeza zinashugulikiwa haraka alisema Naibu Katibu Mkuu.
Upungufu wa Magala ni changamoto nyingine inayoikabili Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirka ambapo, Wizara ina uwezo wa kuhifadhi Tani Laki Mbili na Elifu Arobaini na Moja tu (241,000) katika maghala yote ingawa lengo ni kuwa na uwezo wa kuhifadhi Tani Laki Nne alisema Naibu Katibu Mkuu

 

 

 

 

 

 

 

 

SERIJALI YAJIPANGA KUJENGA KIWADA CHA KUBAGUA KOROSHO

Waziri wa kilimo chakula na ushirika Mh. Chiristopher Chiza amekutana na  wawekezaji wa korosho  kutoka katika taasisi mbalimbali za Maerekani (AFRICA HARVEST OF HOPE)’kujadili uwezekano wa kujenga  kiwanda cha kubangua korosho hapa nchini.
 
Akizungumza na wawekezaji hao amesema kuwa  Serikali ya Tanzania inalikaribisha wazo la kujenga kiwanda cha kubangua korosho   kwa lengo la kuongeza ubora wa zao la korosho ili liweze kupata soko zuri hapa nchini na nje ya nchi.

Aidha Mhe. Naibu Waziri  alisema kuwa, mkulima anapata hasara kwa kuuza korosho gafi hivyo kumfanya apate hasara na kushindwa kuondokana na umaskini.

Katika uwekezaji huo Naibu waziri amewataka  wawekezaji hao  kufanya mabo yafuatayo ili kukamilisha tarabu za uwekezaji, kwanza wakitembelee kituo cha uwekezaji (Tanzania Investment Centre), kwa ajili ya kupata mwongozo wa uwekezaji.

Pia wawekezaji hao wawe tayari kuwashirikisha wakulima katika shughuli zao na wawe tayari kuwa na kilimo cha  mkataba  kitakachomwezesha mkulima kuwa na  uhakika wa kipato chake.

Akiongea kwa niaba ya wenzake Bw. Patrick Chiles alisema kuwa, mradi wao ‘AFRICA HARVEST OF HOPE’ unakusudia kwekeza Tanzania katika zao la korosho, baada ya kuona kuwa zao hili linazalishwa  Tanzania lakini sehemu kubwa inasindikwa  nchini India na kuuzwa nchi zingine, hivyo wameona ni vizuri korosho isindikwe hapa hapa Nchini.

Walitoa ahadi kwamba watafuata taratibu zote za uwekezaji,, kununua korosho nyingi kwa ajili ya kuongeza ajira  ya muda mrefu, ambapo wamesma wamesea pia kuwa  Taasisi yao haitakuwa ya kutengeneza faida kubwa.

 

DRD Yadhamaria Kusajili Watafiti

Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na Maendeleo Dkt. Fidelis  Myaka

 

Idara ya Utafiti na Maendeleo imedhamiria kuweka mkakati wa kuwasajili watengeneza mbegu (Breeders) ili kuwabana wale ambao hawana sifa kama njia ya kuboresha upatikanaji wa mbegu bora.

Azimio hilo lilifikiwa na Wajumbe wa Mkutano wa Kitaifa wa Utafiti wa mbegu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa  Hoteli ya Safari uliopo mjini Arusha hivi karibuni.

Katika Mkutano huo, Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na Maendeleo Dkt. Fidelis Myaka pamoja na Watafiti wengine, wamedhamiria kuanzisha mkakati wa usajili wa wazalisha mbegu baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wakulima na baadhi ya Kampuni za kuzalisha mbegu walidai kuwapo mbegu ambazo  zina kiwango duni na kukosa sifa kadhaa.

Katika usajili huo utaonyesha viwango   vya kitaaluma anavyotakiwa kuwa navyo mzalishaji wa mbegu na  aina za mazao ambazo  anatafiti.

Dkt. Myaka aliendela kusema kuwa Idara itafanya ukaguzi wa Taasisi za utafiti kubaini kama kuna aina za watafiti wasiokidhi viwango ikiwa ni jitihada za kuimarisha uzalishaji wa mbegu. “Kwa kufanya hivi itasaidia kuwarekebisha baadhi ya  Watafiti ambao wanataaluma tofauti na  mbegu wanazozizalisha alisema Dkt. Myaka.

Naye Mwenyekiti wa Mkutano huo Bwana Geoffrey Kirenga amesema Usajili huo utamuweka huru mzalishaji mbegu atakayeamua kuzalisha mbegu tofauti na fani yake kusomea ili kupata taaluma husika, aliongeza kuwa kuwasajili wazalisha mbegu kutaliwezesha taifa kuzalisha mbegu zenye ubora na hatmae kuchangia katika kuinua kilimo alisisitizwa, Bwana Kirenga

 

 

 

Naibu Waziri atembelea Mkoa wa kigoma

Waziri wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Eng. Christopher Chiza akitoa maelekezo kwa mafisa wa wilaya ya Kibondo

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Eng. Christopher Chiza  hivi karibuni alimaliza ziara ya kikazi ya  siku sita katika  Mkoa wa Kigoma katika Wilaya za Kigoma Vijijini, Kibondo,na Wilaya mpya ya Kakonko.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri alifanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa usambazaji pembejeo  ya ruzuku ikiwa ni pamoja  na kupata maelezo na changamoto zilizojitokeza katika utaratibu mzima wa usambazaji wa pembejeo hizo. Moja ya changamoto kubwa iliyoelezwa na baadhi ya wakulima, ni kwa wakulima  kuweka sahihi kwenye vocha bila ya kuchukua  pembejeo husika kutokana na kutokuwa na uwezo wa kulipia  pembejeo zikiwemo mbegu bora na mbolea

Aidha Mhe. Eng. Chiza aliuagiza  uongozi wa wilaya husika  kufanya ufuatiliaji wa karibu katika zoezi  zima la usambazaji wa pembejeo ili kubaini baadhi ya mawakala ambao sio waaminifu. Katika ufuatiliaji huo kila mkulima aliyeweka saini kwenye vocha itabidi athibitishe kuwa alipokea  pembejeo, na kasha kuonyesha shamba lake zilipotumika  pembejeo hizo.

Mhe Eng. Chiza  vile vile alipata fursa  ya kutembelea wakulima wa zao la kahawa katika kijiji cha Muhange , Shughuli za kilimo cha umwagiliaji na katika kijiji cha Nyamtukuza na Kituo  cha mpakani cha Mabamba katika wilaya ya Kibondo kinachoshughulikia  Ukaguzi wa Mazao na Afya ya Mimea.  

Speeches| Publications | Agricultural Statistics | Legislation and Regulations | About us|Contact us
Copyright 2008, Ministry of Agriculture Food Security and Cooperatives All rights reserved.